Breaking News

Your Ad Spot

Feb 16, 2016

"AZMA YA SAUDIA KUIVAMIA SYRIA ILIANZA MIAKA 2 ILIYOPITA"

"Azma ya Saudia kuivamia Syria ilianza miaka 2 iliyopita"
Rais Bashar al-Assad wa Syria amesema mpango wa Saudi Arabia na Uturuki kutaka kuingia kijeshi nchini Syria ulianza miaka miwili iliyopita.
Rais wa Syria aliyasema hayo jana Jumatatu katika matangazo yaliyopeperushwa kwenye runinga ya taifa ya nchi hiyo na kuongeza kwamba, ni kutokana na azma hiyo ndiposa nchi mbili hizo zimekuwa zikiunga mkono harakati za kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh nchini Syria. Rais al-Assad amekariri kuwa, Syria ina hamu ya kuona mgogoro wa nchi hiyo unamalizika haraka, lakini magenge ya kigaidi na waungaji mkono wao hususan Saudi Arabia, wanakwamisha mazungumzo ya kuupatia ufumbuzi mgogoro huo huku akisisitiza kuwa jukumu la kwanza la serikali yake ni kulitokomeza kikamilifu kundi la kitakfiri la Daesh. Kauli ya Rais al-Assad inajiri katika hali ambayo, Saudi Arabia na Uturuki zimesema kuwa huenda karibuni hivi zikaanzisha mashambulizi ya nchi kavu nchini Syria eti kwa lengo la kukabiliana na kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh. Mevlut Cavusoglu, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki amesema Ankara na Riyadh zinajiandaa kwa operesheni ya ardhini nchini Syria na kwamba ndege za kivita za Saudia tayari zimeanza kuingia katika kambi ya Incirlik nchini Uturuki, ambayo kwa sasa inatumiwa na Marekani, Ufaransa na Uingereza katika hujuma zao ndani ya Syria. Wakati huo huo, mshauri wa masuala ya kisiasa wa Rais Bashar al Assad wa Syria amesema kuwa, madai ya Marekani kwamba inapambana na ugaidi ni uongo ulio wazi.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages