Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira
(wapili kulia) akitoka katika Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay,
jijini Dar es Salaam mara baada ya kufungua Warsha ya Kuhamasisha Sheria Mpya
ya Udhibiti wa Silaha na Risasi. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa
Wizara hiyo, Marlin Komba, wapili kushoto ni Naibu Kamishna wa Jeshi la
Polisi-Makao Makuu, Hezron Gyimbi na kulia ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa
Polisi (SACP), Yusuph Ilembo. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akizungumza
na wajumbe wa Warsha ya Kuhamasisha Sheria Mpya ya Udhibiti wa Silaha na Risasi
katika Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam.
Katika hotuba yake, Katibu Mkuu aliwataka watu wanaomiliki silaha nchini isivyo
halali kuzisalimisha haraka iwezekanavyo kabla ya operesheni ya kuwakamata
haijaanza.
Mwakilishi
wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Mawaziri
wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika Mapambano ya Kuzuia na
Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA), Esaka Mugasa akizungumza na wajumbe
(hawapo pichani) wa Warsha ya Kuhamasisha Sheria Mpya ya Udhibiti wa Silaha na
Risasi katika Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es
Salaam. Watatu kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja
Jenerali Projest Rwegasira na wapili kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Sheria
wa Wizara hiyo, Marlin Komba. Katibu Mkuu katika hotuba yake ya ufunguzi wa
warsha hiyo, aliwataka watu wanaomiliki silaha nchini isivyo halali
kuzisalimisha haraka iwezekanavyo kabla ya operesheni ya kuwakamata haijaanza
Sehemu
ya wajumbe wa Warsha ya Kuhamasisha Sheria Mpya ya Udhibiti wa Silaha na Risasi
wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali
Projest Rwegasira
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati
waliokaa), Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara hiyo, Marlin Komba (wapili
kushoto waliokaa), Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi-Makao Makuu, Hezron Gyimbi
(wapili kulia), Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Yusuph Ilembo
(kulia) na kushoto ni Mwakilishi wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na
Pembe ya Afrika katika Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha
Haramu (RECSA), Esaka Mugasa, wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa
Warsha ya Kuhamasisha Sheria Mpya ya Udhibiti wa Silaha na Risasi. Warsha hiyo
ya siku mbili ilifunguliwa na Katibu Mkuu, Rwegasira katika Ukumbi wa Bwalo la
Maafisa wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269