Meneja Masoko wa AccessBank Mr.Muganyizi Jonas Bisheko Akikabidhi Vifaa Mbalimbali kwa Wanafunzi wenye Mahitaji Maalum wanaosoma shule ya Msingi Mtambani Iliyopo Boko Manispaa ya Kinondoni.
Benki
ya Access Bank imetoa Msaada wa Wanafunzi Wenye Mahitaji maalumu
wanaosoma Shule ya Msingi Mtambani Manispaa ya Kinondoni.Meneja Masoko
kutoka Access Bank alisema Msaada huo ni sehemu ya faida ya Benki hiyo
Ambayo Wnarudisha kwa Jamii ya Watanzania hivyo waliguswa na Changamoto
Kubwa Zinazowakabili Wanafunzi hao ikiwwemo Ukosefu wa Miundo mbinu
Rafiki kwajili ya Wanafunzi hao kama Madarasa vyoo na
Vitendea kazi vingine.Akieleza zaidi Bw Muganyizi
Jonas Bisheko Ameomba Makampuni Mbalimbali Kujitokeza Kuwasidia
wanafunzi wao wenye mahitaji Maalum kwa lengo la kuwezesha kupata elimu
Bora kawa Wanafunzi wengine.Benki
hiyo imetoa Vifaa mbalimbali vya kujifunzia pamoja na Michezo kwajili
ya kusaidia kutatua Changamoto zinazowakabili wanafunzi hao
Msaada
huo unajumuisha vitu mbalimbali ikiwemo vifaa vya kujifunzia pamoja na
Michezo,akieleza zaidi Meneja Masoko wa Benki hiyo amesema Accessbenk
imejiwekea utaratibu wa kusaidia jamii ya watanzania hasa kupitia sekta
ya elimu kwa kutatua changamoto zinazoikabili sekta hiyo kama vile
ukosefu wa vifaa na mazingira rafiki ya kuwezesha kutoa elimu bora
Mwalimu
wa shule ya Msingi mtambani anayehusika na Kitengo cha wanafunzi wenye
Mahitaji Maalum akitoa neno la shukrani Mara baada ya Kupokea Msaada
huo.Ameishukuru sana Accessbenki kwa msaada wao amesema kwa kiasi utatua
Changamoto zinazowakabili wanafunzi hao.
Wanafunzi Wenye mahitaji Maalum kutoka Shule ya msingi mtambani walionufaika na msaada huo kutoka accessbenki.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269