Breaking News

Your Ad Spot

Mar 26, 2016

ASKARI WA UN KONGO DR WAUA WAASI WA UGANDA

Askari wa UN Kongo DR waua waasi wa Uganda
Kikosi cha kusimamia amani cha Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo MONUSCO kikishirikiana na jeshi la nchi hiyo kimesema kimefanikiwa kuangamiza idadi kubwa ya waasi wa Uganda mashariki mwa nchi.
Jean Baillaud, Naibu Msemaji wa MONUSCA amesema waasi hao waliuawa katika operesheni ya jana dhidi ya kundi la ADF-Nalu wa Uganda katika kijiji cha Semuliki, karibu na mpaka wa nchi hiyo na Uganda.
Naye Mak Hazukay, Msemaji wa Jeshi la Kongo DR amesema kikosi cha MONUSCO kimeshambulia kwa mahelikopta ngome ya waasi hao mashariki wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Hata hivyo idadi ya waasi waliouawa katika shambulizi hilo haijabainika lakini imearifiwa kuwa raia mmoja aliuawa na wengine watatu kujeruhiwa na waasi wa ADF.
Kundi la waasi la ADF-Nalu lilianzisha uasi na kupanga kuipindua serikali ya Uganda zaidi ya miaka 20 iliyopita, lakini wakalazimika kutorokea DRC. Itakumbukwa kuwa, kwa akali watu 39 waliuawa nchini DRC kufuatia mapigano makali yaliyotokea kati ya jeshi la nchi hiyo na waasi wa ADF-Nalu wa Uganda Disemba mwaka jana 2015.
Eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo limekuwa likishuhudia machafuko kwa zaidi ya miaka 20 sasa kutokana na kuwa ngome ya makundi kadhaa ya waasi kutoka nchi jirani za Rwanda na Uganda.
Baadhi ya vijiji mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo vinadhibitiwa na makundi ya waasi hali ambayo imewafanya wakazi wake kuyaacha makazi yao na kuwa wakimbizi.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages