INAFRIKA BAND AKA “WAZEE WA INDEGE” KUTUMBUIZA MAREKANI (FESTIVAL OF NATIONS)

Bendi maarufu Inafrika band aka
Wazee wa Indege wanatarajiwa kuruka wakati wowote ule kuelekea nchini
marekani kushiriki katika maoyesho makubwa ya kimataifa ya Festival of
nations ,yatakayo fanyika katika Dollywood Theme Park,bendi hii kutoka
Tanzania ndio bendi pekee iliyoteuliwa kuliwakilisha bara la Afrika
katika maonyesho hayo ya kimataifa.
Inafrika band itakuwepo nchini
marekani katika ziara ya kikazi kwa muda wa miezi mitatu kuzikonga nyoyo
za washabiki wa kimataifa nchini marekani.
Kuchaguliwa kwa Inafrika band
kushiriki maonyesho hayo makubwa kunatokana na mvuto wa muziki wa bendi
hiyo kukubalika zaidi kimataifa.
Muziki ambao una maadili ya kitanzania ambako nje ya mipaka umewateka
washabiki wengi wa kimataifa.
Bendi hiyo yenye makao jiji
Dar-es-salaam imejikuta haina muda wa kupumzika kutoka na wingi Tour za
kimataifa kwa muda wa miaka 10 sasa.
Ni kama wiki mbili tu bendi
hiyo imerudi kutoka safari ya nchi 19 za bara la ulaya. Tunawatakia kila
la heri Inafrika Band aka Wazee wa Indege katika kutuwakilisha huko
Marekani. Bendi hiyo ilikuwapo Dollywood ,Marekani mwaka 2014 na
kuwanasa washabiki wengi na muziki wao wa kitanzania
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269