Breaking News

Your Ad Spot

Mar 12, 2016

RAIS DOS SANTOS: KARIBU NITAONDOKA MADARAKANI ANGOLA

Rais Jose Eduardo Dos Santos wa Angola amesema kuwa, ataondoka madarakani mwaka 2018.
Rais Dos Santos ameyasema hayo jana Ijumaa wakati akihutubia wajumbe wa chama chake cha MPLQ na kuongeza kuwa ifikapo mwaka 2018 ataondoka madarakani baada ya kumalizika mihula yote ya uongozi wake.
Muhula wa uongozi wa Rais Jose Eduardo Dos Santos aliyeingia madarakani tangu mwaka 1979, unatazamiwa kumalizika mwaka 2017.
Chama tawala nchini Angola tayari kimeanzisha vikao kwa ajili ya kumuainisha mtu atakayerithi nafasi ya rais huyo.
Hayo yanajiri katika hali ambayo marais wengine wa Afrika wamekuwa wakikataa kuondoka madarakani licha ya katiba za nchi zao kuwabana kufanya hivyo.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages