Breaking News

Your Ad Spot

Mar 27, 2016

WANAJESHI WA BURUNDI WASHAMBULIWA JIJINI BUJUMBURA

Wanajeshi wa Burundi washambuliwa jijini Bujumbura
Watu kadhaa wamejeruhiwa baada ya kutokea shambulio la watu wenye silaha mjini Bujumbura, Burundi.
Shirika la habari la Xinhua limemnukuu Mwese Nkurunziza, naibu wa msemaji wa polisi ya Burundi akisema jana kuwa, wanajeshi wanne wa nchi hiyo wamejeruhiwa. Mmoja wa wanajeshi hao waliojeruhiwa ana cheo cha Kepteni. Wanajeshi hao walishambuliwa kwa guruneti wakati wakipiga doria katika eneo la Musaga, kusini mwa Bujumbura.
Kwa mujibu wa naibu huyo wa msemaji wa polisi wa Burundi, wanajeshi wengine waliokuwepo katika eneo hilo waliwafyatuliana risasi na washambuliaji. Hata hivyo amesema, hakuna mtu yeyote aliyeuawa kwenye ufyatulianaji risasi huo.
Musaga ni moja ya maeneo yenye wapinzani wengi wa serikali ya Rais Pierre Nkurunziza.
Eneo hilo ndilo lililoshuhudia upinzani mkubwa wa kushiriki Nkurunziza katika uchaguzi wa rais wa mwezi Aprili 2015 kwa mara ya tatu mfululizo.
Zaidi ya watu 400 wameripotiwa kuuawa hadi hivi sasa na karibu watu laki mbili na 40 elfu wamekuwa wakimbizi tangu Burundi ilipotumbukia kwenye machafuko yaliyotokana na Rais Nkurunziza kuamua kugombea tena urais nchini humo.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages