Na Mwandishi
Maalum
Wakati Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu upokonyaji wa silaha za maangamizi zikiwamo za
nyukilia kushindwa kwa miaka kumi
na tano kuwasilisha taaria ya mapendekezo ya kina kuhusu utekelezaji wa jukumu
hilo, Tanzania kwa upande wake imeungana na
mataifa mengine katika kutoa
wito wa kuhakikisha kwamba silaha za maagamizi haziangukii mikononi mwa magaidi na makundi mengine
hatari.
Jana Jumatatu, Kamisheni kuhusu
ukoponyaji wa silaha, imeanza mkutano wake wa wiki mbili
ambapo washiriki wanajadiliana na kubadilishana mawazo kuhusu dhima ya
upokonyaji wa silaha za maangamizi na masuala mengine yahusianayo na silaha.
Akichangia majadiliano katika siku ya kwanza ya mkutano , Mwakilishi
wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi, amesema,
utashi wa kisiasa unahitajika hasa
kutoka kwa nchi ambazo zinamiliki silaha za
nyukilia na silaha ninyingine za maangamiii ili kuifanya dunia iendele kuwa mahali salama.
Akabainisha kwamba kutonyesha nia ya
kweli ya kudhibiti malimbikizo ya silaha hizo na, kwa Kamisheni kutowasilisha
mbele ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa
ripoti yake kwa kipindi cha
miaka kumi na tano sasa ni wazi
kwamba kunatoa mwanya wa silaha hizo kuangukia mikononi mwa makundi
ya kigaidi na mengineyo.
Ni katika kuliongopa hilo Tanzania kupitia kwa mwakilishi wake,
Balozi Manongi imeeleza kwamba hoja ya kwamba kwa nchi kumiliki silaha za
maangamizi zikiwamo za nyukilia kunazifanya
nchi hizo kuwa na nguvu lakini pia kujenga mazingira ya Amani kuwa haina tija wala matinki yoyote.
“ Suala la upunguzaji wa silaha za nyukilia na
silaha nyingine za maangamizi ni
jambo linaloitia wasi wasi mkubwa nchi yangu, ni wazi kwamba hatari
zitokanazo na nyukilia ziwe kwa bahati
mbaya, za kimkakati au kukosewa kwa mahesabu siyo tu kunaitishia
dunia lakini pia na wanadamu”. akasema
Balozi na kuongeza kwamba “ Tanzania inaendelea kuikata ile dhana kwamba kwa namna
moja silaha ya nyukilia zinatoa dhamana ya uwepo wa Amani. Kwa upande wetu hatujawahi kujihisi
tukiwa na Amani kwa misingi ya kwamba
silaha hizo amana zinamilikiwa na
rafiki zetu au washirika wao.
Balozi Manongi ametahadharisha kuwa , katika
mazingira ya sasa ambapo
pamekuwapo na ongezeko kubwa
la makundi yasiyo ya kiserikali yanayotaka
kuzipindua serikali halali, hakuna uhakika kwamba makundi hayo hayawezi kugeukia mbinu zozote zile ambazo
zinaweza kuingia mikononi mwao.
Kuhusu Kamisheni ya
Umoja wa Mataifa kutowasilisha
ripoti yoyote mbele ya Baraza Kuu
kwa miaka kumi na
tano, Balozi Manongi asema.
Kamisheni hiyo haiwezi kukwepa majukumu yake
na hasa kama inataka kuendelea
kujijenga uhalali.
“Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, limetoa wito wa kuitaka Kamisheni ifanye tathmini na kutoa
mapendekezo kuhusu matatizo mbalimbali katika eneo hili la upokonyaji wa silaha, na kutoa
maamuzi ya utekelezaji. Mapendekezo ya Kamisheni kwa Baraza Uuu yanatakiwa kutekelezwa na huu ni wajibu wa
msingi wa Kamisheni”. akasisitiza Balozi Manongi.
Pamoja na
mapungufu kwa upande wa Kamisheni,
Tanzania imesema bado na Imani
na Kemisheni hiyo na inaitambua kama chombo pekee halali na
chenye maamuzi katika Umoja wa
Mataifa kuhusu upunguzaji wa silaha
za maangamizi.
Awali akizungumza mwanzoni mwa mkutano wa Kamisheni,
Mwakilishi Maalum wa Masuala ya
upokonyaji wa silaha, Bw.
KIM won-soo, pamoja na mambo mengine alikiri kwamba Kamisheni ilikuwa inaingia katika kipindi kingine ambapo kuna mgawanyiko mkubwa
miongoni wa jumuiya ya kimataifa
kuhusu upokonyaji wa silaha za nyukilia na silaha nyingine za maangamizi.
Akasema kila mjumbe anafahamu kuhusu
mgawanyiko huo. Ambao umejidhihirisha
wazi kuanzia mkutano wa majereo kuhusu Mkataba wa upunguzaji na usambazaji wa silaha za nyukilia ( NPT)
uliofanyika mwaka jana, kushindwa kuanza
kwa utekelezaji wa mkataba unaozuia
majaribio ya silaha za nyukilia, na kutokuwapo kwa mwendelezo wa majadiliano
katika mkutano kuhusu upunguzaji wa
silaha.
Hata hivyo na kama ilivyokuwa kwa wajumbe
wengine, Bw. KIM won –soo alionyesha
matumaini yake kwa Kamisheni ya Umoja wa
Mataifa kuhusu upunguzaji wa silaha za
nyukilia za maangamizi na kwamba wajumbe wake wakifanya kazi kwa pamoja na ushirikiano
na bila kutiliana mashaka hapata kuwa na sababu ya kuwenda kutafuta njia mbadala nje ya Umoja wa
Mataifa.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269