Breaking News

Your Ad Spot

Apr 29, 2016

VIONGOZI WA KISIASA WAFANYA BIASHARA, WATAKIWA KUWAJALI WATOTO WENYE ULEMAVU

 Wanafunzi wa shule ya msingi Mreyai iliyopo wilayani Rombo mkoa wa Kilimanjaro wakisikiliza kwa makini ugeni wa kaimu katibu mkuu uvccm taifa Shaka Hamdu Shaka
 wanafunzi na ugeni ukisikiliza Risala iliyo somwa na mmoja wa wanafunzi walemafu katika shule hiyo
 Kaimu Katibu Mkuu Shaka Hamdu Shaka akipokea Risala ya Wanafunzi
 Mkuu wa shule ya msingi Mreyai Nuruel Laizer  wa kwanza kushoto akifuatiwa na mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa kilimanjaro Juma Rahibu Juma akifuatiwa na kaimu  katibu mkuu UVCCM taifa katika makabidhiano ya baadhi  ya msaada ambao ulipelekwa shuleni hapo
 Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka alizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mreyai
 Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka alizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mreyai
 Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka H Shaka akizungumza na moja ya Wanafunzi wenye ulemavu
 Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka H Shaka akipanda mti
Wanafunzi wa Shule ya msingi Mreyai wakifurahi pamoja na 
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka  Shaka.

===================

NA FAHADI SIRAJI
Viongozi wa kisiasa, wafanyabiashara, viongozi wa kiserikali na wafanyajazi wametakiwa kuwajali na kuwathamini sana watoto  wenye ulemavu na wanaoishi kwenye mazingira magumu kwani wao pia  ni binadamu wanao sitahili kupata haki na mahitajj muhimu ya kibinadamu.

Hayo yamebainishwa na leo na kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka wakati alipotembelea shule ya msingi Mreyai iliyopo wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro yenye jua huduma watoto wenye ulemavu wa viungo na mtindio wa akili.

Alisema kuwa ni muhimu kuwajali sana watoto wenye ulemavu kwani wakitengenezwa vizuri na kuandaliwa vizuri kwa kupewa elimu  watakuwa viongozi wazuri wa baadae.

Aidha alivitaka vyama Vya siasa vijielekeze kutatua changamoto na ma tatizo ya watoto ambao ni Walemavu na sio kuendeleza Kufanya siasa ata sehemu
ambayo aitakiwi siasa.

"napenda kuviambia vyama vingine vya siasa sasa ivi uchaguzi imeisha ni kipindi cha kufanya kazi na kuachana na siasa sasa ivi ni kipindi cha kufanya kazi na kutatua ma tatizo ya wananchi " alisema Shaka.

Kwa upande wa Mkuu wa shule ya msingi Mreyai, Nuruel Laizer alisema kuwa shule hiyo inahudumia wanafunzi wenye Mtindio wa akili na wanafunzi ambao ni walemavu wa viungo ambapo alisema kuwa shule hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya ukosefu wa chakula cha wanafunzi, ukosefu wa vitanda na mgodoro ya kulalia Wanafunzi ambao ni walemavu ,baskeli kwa
ajili ya watoto ambao ni walemavu wa miguu.

Alisema kuwa Wanafunzi hao wanakaa katika ma bweni apo shule ni lakini wanaupungufu mkubwa wa vitanda na mgodoro  kwani vitanda ambavyo wana vitu mia wameviazima kutoka kwa watu na mda wowote wenyewe wanaweza kuja kuchukuwa.

Aliomba serekali pamoja na wadau mbalimbali kujitokeza kuwasaidia kitu icho ili watoto hao waweze kuishi kwa amani na furaha kama watoto.

"watoto hawa wanawazazi lakini wazazi hao hawana uwezo na ndio maana wa me wamewaleta Hapa ili wapate elimu hivyo tu naomba sana serekali na wadau mbalimbali wajitokeze kutusaidia"alisema Laizer

Shule hii ya msingi Mreyai imepata msaada wa chakula, maharage, malindi, sabuni, mafuta, miswaki na kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka aliaidi kusaidia shule hii vitanda Nane na mgodoro kwa ajili ya wanafunzi hawa wenye ulemavu wa viungo pamoja na Mtindio wa ubongo.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages