Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles
Kitwanga akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Jimbo
lake mara baada ya Mbunge huyo kutoa msaada wa Baiskeli 120 zenye
thamani ya zaidi ya shilingi milioni 22 kwa ajili kutumika jimboni humo
katika shughuli mbalimbali za chama. Makabidhiano hayo yalifanyika
katika Ofisi ya CCM Wilaya ya Misungwi ambapo makatibu wote wa matawi
walikabidhiwa baiskeli hizo.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM), Mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu akizungumza na Wanachama wa CCM wa
Jimbo la Misungwi mara baada ya Katibu huyo kukabidhiwa Baiskeli 120
zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 22 na Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo hilo, Charles Kitwanga
(wanne kulia mstari wa mbele). Baiskeli hizo walikabidhiwa makatibu wote
wa matawi wa CCM jimboni humo ili ziweze kurahisisha usafiri katika
kazi mbalimbali za chama jimboni humo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles
Kitwanga (kulia) akimkabidhi Baiskeli 120 zenye thamani ya zaidi ya
shilingi milioni 22, Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa
Mwanza, Miraji Mtaturu kwa ajili ya kuwakabidhi makatibu wa matawi wa
CCM Jimbo la Misungwi ili ziweze kutumika kwa ajili ya shughuli za chama
jimboni humo. Makabidhiano hayo yalifanyika katika Ofisi ya Wilaya ya
Chama hicho, mjini Misungwi.
Katibu
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu (kushoto)
akiwakabidhi Baiskeli baadhi ya makatibu wa matawi wa CCM wa Jimbo la
Misungwi, mara baada ya Katibu huyo kukabidhiwa Baiskeli 120 zenye
thamani ya zaidi ya shilingi milioni 22, na Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo hilo, Charles Kitwanga (kulia).
Baiskeli hizo ambazo zitatumika katika shughuli za kichama jimboni humo
zilikabidhiwa katika ofisi za chama hicho, mjini Misungwi leo.
Picha zote na Felix Mwagara.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269