Breaking News

Your Ad Spot

May 29, 2016

BURUNDI NA MOROCCO KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIBUNGE BAINA YAO

Spika wa Baraza la Seneti nchini Burundi ameelezea habari ya safari ya Spika wa Bunge la nchi hiyo, Révérien Ndikuriyo nchini Morocco katika kukamilisha ushirikiano wa pamoja wa kibunge baina ya nchini hizo mbili.
Stella Budiriganya, msemaji wa Baraza la Seneti la nchi hiyo ameviambia vyombo vya habari kwamba, Ndikuriyo alifanya safari nchini Morocco Jumamosi ya jana katika fremu ya kuimarisha ushirikiano uliopo kati ya bunge la nchi hiyo na lile la Burundi. Aidha Bi. Stella Budiriganya ameongeza kuwa, bunge la seneti la nchi Burundi linaisaidia serikali katika kufanikisha siasa kuu za kitaifa nchini humo. Hii ni katika hali ambayo, katika safari yake nchini Burundi hapo tarehe 28 Machi mwaka huu, ujumbe wa bunge la Morocco ulisisitiza kuwa wanaharakati wa kiuchumi wa Morocco watafanya safari hivi karibuni mjini Bujumbura kwa lengo la kutathmini uwezekano wa kuwekeza katika sekta tofauti nchini humo. Kadhalika kamati ya bunge la Morocco ilisema kuwa, shirika moja la ndege la nchi hiyo litaanza kufanya safari za moja kwa moja baina ya Bujumbura na Casablanca.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages