Breaking News

Your Ad Spot

May 23, 2016

LIBYA YAUOMBA UMOJA WA ULAYA UISAIDIE KULINDA FUKWE ZAKE

Serikali ya Libya imeuomba Umoja wa Ulaya uisaidie kulinda fukwe zake kupitia kutoa mafunzo kwa jeshi la majini la nchi hiyo.
Shirika la habari la Sputnik News la Russia limemnuukuu Bi Federica Mogherini, Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya akisema hayo na kuongeza kuwa, viongozi wa Libya wameuomba rasmi umoja huo uwape mafunzo maafisa wake wa jeshi la majini kama njia ya kuisaidia kulinda mipaka yake.
Mogherini amesisitiza kuwa, hatua hiyo ya viongozi wa Libya ni muhimu sana.
Ombi hilo la viongozi wa Libya lilitarajiwa kuwa moja ya ajenda za kikao cha leo Jumatatu cha Baraza la Ulaya na ilitarajiwa kuwa, baada ya kujadiliwa ombi hilo, kuchukuliwe hatua za lazima za kuwasaidia wananchi wa Libya.
Siku ya Ijumaa pia, Mogherini alisema kuwa, Umoja wa Ulaya na jumuiya ya kijeshi ya NATO zinaweza kuisaidia Libya kupitia kutoa mafunzo kwa maafisa wake wa kijeshi wanaolinda fukwe za nchi hiyo kwa shabaha ya kupambana na magendo ya silaha katika Bahari ya Mediterranean.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages