Breaking News

Your Ad Spot

May 4, 2016

MISRI YAREJEA KWENYE BUNGE LA AFRIKA BAADA YA KUTENGWA KWA MUDA MREFU

Hatimaye Misri imerudi kwenye bunge la Afrika baada ya kutengwa kwa kipindi cha miaka mitatu.
Gazeti la Misri la al-Watan limeandika kuwa ujumbe wa Misri ukiongozwa na spika wa bunge la nchi hiyo Ali Abdul-Aal, umehudhuria kikao cha bunge la Afrika mjini Johannesburg, Afrika Kusini na kwa utaratibu huo, nchi hiyo ikawa imerejea rasmi kwenye bunge hilo. Hatim Bashat, Salah Aqiq, Mustafa Jundi, Mayi Mahmoud na Sayyid Falifel, ni shakhsia walioandamana na spika wa bunge la Misri kwenda mjini Johannesburg ambapo pia walipata kuapishwa na bunge la Afrika. Katika sherehe hizo za kuapishwa, Mahmoud amesema kuwa, vikao vya bunge la Afrika ni fursa muhimu kwa ajili ya Cairo kuweza kurejea kwenye taasisi hiyo muhimu barani Afrika. Bunge la Afrika ni moja ya taasisi zilizo chini ya Umoja wa Afrika ambalo liliasisiwa mwezi Machi mwaka 2014. Misri ilienguliwa katika bunge hilo baada ya mapinduzi ya kijeshi dhidi ya Rais Muhammad Mursi, hatua ambayo ilifuatiwa na kuvunjwa bunge la nchi hiyo na makamanda wa jeshi wanaotawala nchi hiyo hivi sasa.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages