Breaking News

Your Ad Spot

May 27, 2016

MSEMAJI WA WIZARA YA MABO YA NJE YA IRAN AMJIBU ADEL AL JUBEIR

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani matamshi ya kuivunjia heshima Iran yaliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia.
Sadeq Hussein Jaberi Ansari, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran leo amejibu matamshi ya uvunjaji heshima ya Adel al Jubeir kuhusu uhusiano kati ya Iran na Iraq na kueleza kuwa, taifa la Iraq halina haja na matamshi ya waziri wa Saudia ambayo katika kipindi cha karibu muongo mmoja na nusu wa hivi karibuni imekuwa chanzo kikuu machafuko na ugaidi huko Iraq, katika eneo la Mashariki ya Kati na ulimwenguni kwa ujumla. Jaberi Ansari ameongeza kuwa, kuwepo washauri wa kijeshi wa Iran huko Iraq chini ya uongozi wa Kamanda Qassim Suleimani kumefanyika baada ya serikali ya Iraq kuiomba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iitumie washauri wa kijeshi katika juhudi zake za kupambana na magaidi na makundi yenye misimamo ya kufurutu ada, ambayo yamevuruga amani na utulivu wa Iraq na eneo hili zima. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amemtaka Adel al Jubeir asisahau kuwa nchi yake inatambuliwa kimataifa kuwa ndiye muungaji mkono mkuu na hatari zaidi wa ugaidi na kwamba ndiyo nchi inayosabaabisha kuenea machafuko duniani, badala ya kujaribu kila awezalo kuzihadaa fikra za waliowengi na kupotosha uhakika wa mambo. Adel al Jubeir Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia jana alidai katika mahojiano na televisheni ya Russia al Yaum kuwa eti Iran inaingilia masuala ya ndani ya Iraq.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages