Nyegere |
NYEGERE ni moja kati ya wanyama wanaoelezwa kuwa wenye wivu sana hapa duniani ambapo wachuncguzi wa masuala ya sayansi za wanyama, wanadai kwamba chakula chake kikubwa ni asali.
Inaelezwa kwamba, Nyegere hupanda juu ya mzinga wa asali na kuujambia na baada ya mashuzi yake nyuki wote hulewa na yeye kupakua asali na masega yake na kisha kula.
Ujasiri wa kuingia kwenye mizinga ya nyuki na kushambulia kwa masuzhi unasaidiwa na mwili wake wenye ngozi ngumu sana kiasi hata nyuki hawawezi kumdunga akaadhirika kwa lolote kama inavyotokea kwa wanyama mbalimbali na binadamu.katika tukio moja inadaiwa mkoani Singida aliwahi kusafiri zaidi ya kilomita saba usiku kwa usiku anafuata harufu ya mtu aliyerina mzinga wa asali aliyoijambia, alipofika akavunja mlango na kukuta wamelala watu wanne kwenye mkeka mmoja,akabagua yule mwizi wake, akagawa kichapo halafu akarudi porini kimya kimya.
Nyegere anaweza kununua ugomvi mpaka kijiji cha sita, warina asali ndio waathirika wakubwa wa hasira za Nyegere,anaweza kuujambia mzinga akala kidogo asali na kupeleka kwa mke ,mrina asali akifika na kupakua, nyegere ana uwezo ya kufuatilia harufu ya aliyeiba asali yake mpaka nyumbani, na akifika anavunja mlango na kuingia ndani na kumvamia mwizi wa asali yake(ukizingatia milango ya vijijini si imara). Watu wengi vijini wameuwawa kwa namna hii.
Mnyama huyu Nyegere ni mnyama mwenye wivu na mapenzi makubwa sana kwa jike lake, hutembea nyuma ya jike huku akiwa ameziba sehemu za siri za jike, hata jani tu likiigusa sehemu ya siri ya jike litararuliwa na kupokea kichapo cha hatari,maana wivu wake ni kuwa jani laitakuwa "limefaidi utamu" wa jike.
Wivu wa Nyegere hufanya awachukie sana hata binadamu wanaume, mwanaume akiwa porini akakutana na Nyegere akiwa na jike lake basi ajiandae kupata kibano, huona wivu kuwa utamtamani jike, hivyo hukimbilia kumvamia mwanaume sehemu za siri akiamini ndizo zinazokupa jeuri ya kumtamani jike lake.
Nyegere ndio mmoja kati ya "fearless animal" duniani, huweza kuwakabili Simba na Chui zaidi ya mmoja na kuwashinda,anasaidiwa na ngozi yake ngumu na kucha zake, awapo katika hatari ya kushambuliwa hukakamaa na ngozi yake kuwa ngumu kama "defensive mechanism" yake.
Kuna baadhi ya makabila ambayo inasemekana waganga wa kienyeji hutumia mchanganyiko wa Nyegere kutengenezea limbwata,Yaani wamama huchukua dawa hiyo kuwawekea waume zao ili wawe na "upendo" wa Nyegere.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269