Breaking News

Your Ad Spot

May 21, 2016

PAZIA LIGI KUU YA VODACOM KUFUNGWA KESHO

Michezo ya mwisho ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, inatarajiwa kufanyika kesho Jumapili, Mei 22, 2016 kwa timu zote 16 kutinga katika viwanja vinane tofauti kumaliza ngwe ya msimu wa 2015/16.
Michezo itakayopigwa kesho ni pamoja na Simba itakayokipiga na JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Azam FC ambayo inawania nafasi ya pili kama Simba, itakipiga na African Sports kwenye Uwanja wa Azam Complex, ulioko Chamazi, Mbagala nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga ya Dar es Salaam inakaribishwa Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa Majimaji mjini humo ilihali Mwadui na Kagera Stars zitamaliza ligi katika Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Kadhalika kwa mujibu wa ratiba hiyo ya Ligi Kuu ya Vodacom, Toto Africans itakuwa mwenyeji kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kuikaribisha Stand United, wakati African Sports ‘Wanakimanumanu’ wameifuata Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Manungu, Mvomero mkoani Morogoro.
Mechi nyingine ya kukunja jamvi kwenye Ligi Kuu ya Vodacom zitakuwa kati ya Mbeya City dhidi ya Ndanda FC ya Mtwara huku mchezo mwingine wenye presha utakuwa ni kwa Tanzania Prisons yenye pointi 48 ambayo licha ya kucheza na Coastal Union ambayo tayari imeshuka daraja kwenye Uwanja wa Mkwakwani, itakuwa inafukuziwa na Mtibwa Sugar kuwa na nafasi ya nne. Mtibwa Sugar ina pointi 47 na mvutano ni wa nafasi ya nne hasa ukirejea kwenye zawadi za Vodacom za Vodacom.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages