Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli ametangaza
kushusha kodi ya mapato ya Mshahara ( Pay as you Earn -PAYE ) kutoka
asilimia 11 iliyopo sasa hadi asilimia 9.
Rais
amesema ameamua kuchukua umamuzi huo ili kutimiza ahadi yake aliyoitoa
wakati wa kampeni ya kuwapunguzia mizigo wafanyakazi kwa kuwaongezea
mishahara na kuwapunguzia kodi ya mapato ya mishahara.
Kuhusu
kuwaongezea mishahara, Rais Magufuli ameomba wafanyakazi wamvumilie kwa
kuwa hivi sasa yuko kuimarisha uchumi wa nchi kwa kuziba mianya yote ya
Rushwa.
Katika
hatua nyingine, Rais Magufuli amewataka waajiri wote nchini kuwapa
wafanyakazi wao mikataba ya ajira na kupeleka makato yao kwenye mifuko
ya hifadhi ya jamii bila kukosa
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269