Breaking News

Your Ad Spot

May 4, 2016

TANZANIA YATAKA MKUTANO WA MASUALA YA KIBINADAMU DUNIANI UWE WENYE TIJA

Na Mwandishi Maalum
Wakati   Jumuiya ya Kimataifa  ikielekea kukamilisha maandalizi ya Mkutano Maalum wa Kimataifa kuhusu Masuala ya Kibinadamu, ( World Humanitarian Summit)  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa upande wake,  imesema ,  ni matarajio yake kwamba mkutano huo unatatoka na  makubaliano yanayotekelezeka.
Kauli  hiyo  imetolewa siku ya Jumanne , na Balozi  Tuvako Manongi, Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, wakati yeye na  Mwakilishi  wa  Kudumu wa Denmark Balozi Ib Petersen , walipoongoza majadiliano  yasiyo rasimi kuhusu uzibaji wa  mgawanyiko kati ya  mahitaji ya kibinadamu na  maendeleo; kutoka nadharia kwenda kwenye vitendo. Mkutano huo uliandaliwa   Mfuko wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa ( UNDP).
“Mkutano  ujao ni  fursa nyingine kwa Jumuiya ya Kimataifa ya kuonyesha utashi wa kisiasa,  kujadili kwa kina na tija changamoto zinazohusu ubinadamu na  misaada ya kibindamu,  ni fursa  inayotakiwa kutumiwa vema katika utoaji wa ahadi na utekelezaji wa ahadi hizo kwa vitenda pasipo kumwacha yeyote nyuma”. Akasema Balozi Manongi.
Na kuongeza kuwa  ingawa  Tanzania kama nchi ambayo kwa maiaka  mingi imekuwa ikiwapokea, kuwahifadhi na  kutoa misaada ya  kibinadamu  kwa wakimbizi kutona nchi jirani,  inautizama mkutano  huo wa Instambul katika sura mbili  tofauti.
Akasema moja ya  sababu ambayo  Tanzania inautizama kwa sura tofauti  mkutano huo wa  Instambuli  kwamba umuhimu unaopewa mkutano huo, unakizana na  umuhimu ambapo nchi kama Tanzania na nyingine hazikupewa au hazipwewi pale  zinapokabiliwa na  changamoto kubwa ya  kuwawapokea  na kuwahifadhi wakimbizi   kutoka nchi jirani.
“  Tanzania  tumekuwa kwa miaka mingi  tukihifadhi wakimbizi,  na katika miaka  ya 90 tulipata changamoto kubwa  sana ya  kuwapokea na kuwahifadhi wakimbizi kutoka nchi jirani,  matarijio  yalikuwa ni kuona  mwitikio wa haraka lakini  haikuwa hivyo. Ushirikiano  tulioupata ulikuwa wa    kutoka Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa na  Nchi  za Scandinavia”. Akasema Balozi.
Mkutano wa  masuala ya kibinadamu umeitishwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban  Ki Moon,    utafanyika kati ya 23 na 24 mwezi huu wa March  huko  Instambul –Uturiki   na  unatarajiwa kuhudhuriwa na  Viongozi wakuu wa nchi na Serikali,  Taasisi na Mashirika  ya  Kimataifa yahusikayo na  misaada ya kibinadamu .
Ni mkutano unaofanyika katika  kipindi ambacho pamekuwapo na wimbi kubwa la  maelfu  ya wakimbizi wanaokimbia machafuko na vita katika nchi zao na kukimbilia nchi  za  Ulaya kutafuta hifadhi. Huku mamilioni wengine wakiwa ni wakimbizi wa ndani  au wamekimbilia nchi   jirani.


Balozi  Manongi,Akabinisha pia   kwamba hata katika Taarifa ya Katibu Mkuu inaonyesha kuwa bado kuna mapengo katika  kughughulikia   utoaji wa misaada ya kibinadamu, mapengo ambayo yanatakiwa kufanyiwa kazi kwa kuanzia kwa watoaji wa misaada, wasambazaji wa misaada hiyo  hadi kwa walengwa wa misaaada hiyo. Na  Akasisitiza  Mkutano huo wa Instambul utatoa nafasi ya kujitizama upya na angalau  kujafa jambo litakalo weza kuchangia kubadili hali  ya sasa.
Mwakilishi  huyo wa Tanzania,  amewaeleza washiriki wa mkutano huo,   licha ya kufanyika kwa mkutano mbalimbali  ya  kimataifa  ukiwamo wa 2012 kujadili  majanga ya kibinadamu,  bado majanga hayo yanaendelea kuwapo huku  ongezeko la  hitajio la  misaada ya kibinadamu likiendelea  kuongezeka.
Akaeleza  kwamba si kweli kuwa  hakuna watu au wadau wenye mapenzi mema na wanaotaka kusaidia. Bali  kinachotakiwa ni namna gani  nchi zinazopata matatizo zinashirikianaje  na  kwa pamoja na   Umoja wa Mataifa, na  wadau mbambali katika kuyakabili  matatizo hayo.
Balozi Manongi amebainisha pia kwamba  Tanzania   ingepeda  kuona mkutano huo  unatoka na mapendekezo yenye tija ya namna ya kumaliza migogoro na vita na ulinzi wa  binadamu  kwa kile  alichosema  asilimia 80 ya   masuala ya kibinadamu na ubinadamu  chanzo chake ni  migogoro na vita.
Katika  mkutano huo ambao Balozi  Manongi na Balozi Petersen waliongoza   nchi za Ethiopia,  Pakistani na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo  zilielezea uzoefu wao na changamoto katika kuyakabili  majanga ya kibinadamu  yakiwamo yatokanayo  na mabadiliko ya   tabia nchi, ukame na mafuriko,  vita na machafuko na uhifadhi wa wakimbizi kutoka nchi jirani.
Nchi hizo zilieleza namna serikali kama zenyewe  na  kwa ubia na mashirika  ya kimataifa na  wadau  wa maendeleo pamoja na wananchi walengwa ambavyo kwa umoja wao wameweza  kutekeleza sera  na mipango ya kujiandaa kwa maafaa kabla ya hayajatokea, namna zinavyo kabiliana na  maafaa hayo yakisha tokea na baada ya kutokea.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages