Jumuiya ya
vijana UVCCM imetoa wiki moja kwa wale wote waliouza
viwanja na rasilimali za jumuiya hiyo kujiandaa kwa ajili ya
kupelekwa mahakani .
Agizo hilo
limetolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM taifa Shaka Hamdu
Shaka wakati akiongea na viongozi wa umoja huo wakiwemo
wenyeviti wa mikoa ,wenyeviti wa wilaya pamoja na makatibu wa
umoja huo kutoka katika mikoa ya Arusha ,kilimanjaro pamoja na manyara
waliokutana katika ofisi ya CCM wilaya moshi mjini katika
majumuisho ya ziara yake alikuwa akifanya katika mikoa
hiyo.
Alisema
kuwa baadhi ya watu wamegeuza mali za jumuiya hiyo kama shamba la bibi
kwani kila mtu amaekuwa akitumia mali hizo na kuzitawanya kama
anavyotaka hivyo ataakikisha anawachukulia hatua kali za kisheria kwa
kuwapeleka mahakamani wale wote ambao wamehusika kufanya
hivyo.
Alibainisha kuwa kwa sasa hivi katika uongozi wake
amethamiria kuimarisha jumuiya hiyo ,na hata pepesa
macho kwa yeyote yule wala kumuonea huruma yeyote yule ambaye
amezifanya mali hizo za jumuiya
kama shamba la bibi.
"nasema
lazima nitampeleka mtu mahakamani ambaye atachezea mali za
jumuiya kwani sasa ivi watu wengi wamegeuza jumuiya
kama yao sasa nasema hivi nita kula nao sahani moja bila
kuwaonea haya wala aibu tunataka kazi ambazo zinafanywa na jumuiya hii
zionekana na watu wasione jumuiya hii kama mzigo ,tunataka kazi
zinazofanywa na jumuiya zitambulike na tusiwe kama mzigo ndani ya
chama sisi ni vijana tunanguvu ,uwezo tunao tukiamua kufanya kwa
moyo na kwa nguvu zetu zote"Alisema Shaka.
Pia kwa
upande wa utendaji ndani ya Jumuiya hiyo alisema kuwa kwa
mtendaji yeyote ambaye anaona awezi kwenda na mabadiliko na kasi
anayoitaka aachie ngazi mapema kabla ajamkuta maana atamuonea
huruma yeyote kwani awataki watendaji wavivu wala mizigo ndani ya
chama .
"napenda
kusema kwa upande wa watendaji aijalishi wewe ni mwenyekiti
,katibu au hata katibu hamasa ukiona uwezi kuifanyia kazi chama
achiangazi mapema tuandikie tuambie umeshindwa kazi dai mafao yako
uondoke mapema kabla atujakukuta maana tukikukuta atuna cha salia
mtume lazima tutakutoa narudia tena atutaki viongozi mizigo tunataka
viongozi ambao wanafanya na wanafanya kitu kinachoonekana sio wanakaa
tu ofisini kula kiyoyozi"alisema Shaka .
Alibainisha
kuwa muda wa majungu ,fitina ,umbea na poroja umeisha na sasa ivi
kinachoitajika ni mabadiliko ya utekelezaji wa majukumu ya
kazi za kila siku kufuata vikao vya kikanuni na kubuni
miradi ya maendeleo na itayokuza uchumi kwani UVCCM
anayoitaji kwa sasa ni ya siasa na uchumi huku akiziagiza wilaya zote
na mikoa kubuni miradi mbalimbali ya maendeleo.
wabibi waliouthuria mkutano wa shaka w wakiwa
wanateta jambo
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269