Waziri
wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Hamad Rashid Mohammed ambae
alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya Wakunga Duniani
akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Baraza la Wauguzi na Wakunga
Zanzibar Profesa Amina Abdulkadr, (kulia) Waziri wa Afya Mahmoud Thabit
Kombo na (kushoto) Naibu Katibu Mkuu Wizara hiyo Halima Maulid Salum.
Mwenyekiti
wa Baraza la Wauguzi na Wakunga Zanzibar Profesa Amina Abdulkadr
akisoma risala ya wakunga katika maadhimisho ya siku ya Wakunga Duniani
yaliyofanyika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Mjini Zanzibar.
Mwakilishi
wa Shirika linaloshughulikia Idadi ya watu (UNFPA) akitoa salamu za
Shirika hilo kwenye maadhimisho ya siku ya Wakunga Duniani yaliyofanyika
Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Mjini Zanzibar.
Waziri
wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akimkaribisha Mgeni rasmi Waziri wa
Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Hamad Rashid Mohammed katika
maadhimisho ya siku ya Wakunga Duniani.
Waziri
wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Hamad Rashid Mohammed akionyesha
vitabu viwili vya maadili ya wakunga na wauguzi alivyovizindua katika
maadhimisho ya siku ya Wakunga Duniani.
Waziri
wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Hamad Rashid Mohammed akihutubia
Wakunga walioshiriki maadhimisho ya siku ya Wakunga Duniani
yaliyofanyika Ukumbi wa sanaa Rahaleo Mjini Zanzibar.
Mwakilishi
wa Jumuia ya CHARA (katikati) akiongoza kukata Keki ya maadhimisho ya
siku ya Wakunga Duniani yaliyofanyika Ukumbi wa sanaa Rahaleo Mjini
Zanzibar.
Picha na Makame Mshenga-Maelezo.
………………………………………………………………………………………..
Makamo wa Pili wa Raisi wa
Zanzibar Balozi Seifu Ali Iddi amewataka Wakunga na Wauguzi kutoa
huduma bora kwa mama wajawazito bila kujali misingi ya Dini,Kabila,Rangi
wala itikadi za kisiasa ili kuwajengea imani na kupenda kujifungulia
hospitali na vituo vya afya.
Akisoma hotuba kwa niaba ya Makamo
wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Waziri wa Kilimo,Maliasili Uvuvi na
Mifugo Hamad Rashid Muhammed amesema wauguzi ni watu muhimu hivyo ni
vizuri kutumia taaluma yao kwa kuzingatia misingi ya maadili ya maadili
ya kazi hiyo.
Amesema pamoja na Wauguzi
kufanyakazi katika mazingira magumu amewataka kufanyakazi kwa uzalendo
na uadilifu ili kuwanusuru Wanawake kupta matatizo wakati wa kujifungua
yakiwemo kupoteza Damu nyingi wakati wa kujifungua na kupata kifafa cha
mimba.
Amefafanua kuwa wajawazito
wanahitaji kupata Uangalizi wa karibu kabla na wakati wa kujifungua
hivyo hakuna budi kwa Wakunga kuwa pamoja nao kupata msaada wao .
Hamad Rashid ameshauri kutokana
na kazi kubwa wanazofanya Wakunga na Wauguzi hakuna budi kuingizwa
katika Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ili waweze kuwa na uhakika wa
Maisha yao.
Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud
Thabit Kombo amesema umuhimu wa kazi za Wakunga zinaonekana na kila
mtu na wanapofanya vizuri idadi ya vifo vya mama wajawazito na watoto
itaendelea kupungua.
‘’Kazi yenu ni muhimu na mimi na
mh. Hamad Rashid kama musingetekeleza kazi yenu vizuri tusingezaliwa,’’
aliongeza Waziri Mahmoud.
Ameyashukuru mashirika ya
kimataifa yanayosaidia sekta ya Afya wakiwemo WHO, UNICEF na Mashirika
mengine kwa michango yao mikubwa wanayotoa kwani amesema asilimia kubwa
ya Mipango ya Bajeti ya Serikali katika Wizara ya Afya inategemea
michango kutoka kwao.
Mapema akisoma Risala ya Siku ya
Wauguzi Duniani Mwenyekiti wa Baraza la Wauguzi na Wakunga Zanzibar
Prof. Amina Abdul-kadir amesema Zanzibar imefanikiwa kupunguza idadi ya
vifo vya mama wajawazito kutoka 285 mwaka 2011 na kufikia vifo 187
mwaka 2014 baada ya akinamama wengi kuwa na mwamko wa kujifungulia
katika Hospitali na vituo vya Afya.
Ameongeza kuwa huduma mbali mbali
zimechukuliwa ikiwemo uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi na
matiti na kufanya majadiliano juu ya huduma mbali mbali zinazowahusu
wakunga na wauguzi.
Aidha amesema kumekuwa na
changamoto katika kupata ufanisi mzuri zaidi ikiwemo uhaba wa wataalamu
wa fani ya uuguzi, Uhaba wa Vifaa vya kufanyiakazi, Mishahara midogo na
Mazingira magumu ya kufanyia kazi.
Ujumbe wa mwaka huu katika
maadhimisho ya siku ya Wakunga Duniani ni Wanawake na Watoto wachanga
muhimili wa ukunga kwa pamoja tuepushe vifo vya mama na mtoto.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269