
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika mashariki Balozi Augustine Maiga akitoa maelezo kwa wadau waliohudhuria mkutano wa Utawala wa Sheria na Utawala Bora (hawapo pichani) uliofanyika leo jijini Dar es salaam

Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustine Maiga
akiongea jambo na Balozi wa Italia Nchini Mhe. Luigi Scotto baada ya kumaliza
mkutano wa Utawala wa Sheria na Utawala Bora uliofanyika leo jijini Dar es
salaam.

Wadau
wa Mkutano wa Utawala wa Sheria kutoka nchi mbalimbali duniani wakifatilia kwa
makini mkutano wa Utawala wa Sheria na Utawala Bora ili kufikia agenda ya mwaka 2030 na 2063 ya
malengo ya millennia uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
Picha
na Ally Daud- Maelezo
Afrika
yatakiwa kuimarisha Utawala wa Sheria: Balozi Mahiga
Na:
Immaculate Makilika- MAELEZO, Tarehe 02/06/2016
Dar
es Salaam
BARA
la Afrika limetakiwa kuimarisha Utawala wa Sheria kupitia vyombo vya dola
ikiwemo mahakama na polisi ili kuisaidia
mfumo huo kutetea maslahi ya wanyonge.
Hayo
yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Balozi Augustine
Mahiga wakati alipokuwa akifunga Mkutano
wa siku mbili wa Kimataifa kuhusu
Utawala wa Sheria na Utawala bora.
“Lazima
Afrika iimarishe vyombo vyake vinavyosimamia Utawala wa sheria na Utawala bora kama
Polisi na Mahakama pamoja na kuwa na msimamo wa Bara katika kuzungumzia masuala
mbalimbali” alisema Balozi Mahiga
Balozi
Maiga alisisitiza kuwa rushwa imekua adui mkubwa katika Utawala wa Sheria,
hivyo ni lazima suala hilo lipatiwe ufumbuzi ili haki iweze kutendeka kwa watu
wote.
Aidha,
Balozi Maiga amemshukuru Balozi wa Italia nchini Mhe. Luigi Scott kwa
kufanikisha mkutano huo pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la
Maendeleo ya Sheria (IDLO) Bibi. Irene Khani kwa uamuzi wa wake wa kuichagua
Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano huo.
“Mkutano
huu ni wa kihistoria utasaidia kuleta mageuzi katika Taasisi ama Vyombo
vinavyosimamia masuala ya Sera na Sheria ambayo yatachochea maendeleo mazuri
katika nchi za Afrika” alisema Balozi Mahiga.
Mkutano
huo unaomalizika leo ulikua na kauli mbiu isemayo “Kufikia agenda ya 2030 na
agenda ya 2063: Utawala wa Sheria kwa Maendeleo Endelevu ya Afrika”, umehusisha
wadau mbalimbali wakiwemo Mawaziri, kutoka nchi mbalimbali za Afrika, Mabalozi
kutoka ndani na nje ya Afrika pamoja na wawakilishi wa Mashirika ya kutetea
Haki za Binadamu ulimwenguni.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269