Na Mwandishi Maalum, New York
Imeelezwa kwamba , upatikanaji wa
vifaa saidizi ( assistive divices) kwa
watu wenye ulemavu wa aina
mbalimbali siyo tu, utawawezesha kushiriki katika shughuli za
kiuchumi, kijamii na maendeleo bali pia utawaondolea hisia za kunyanyapaliwa na kubaguliwa.
Hayo
yameelezwa na siku ya jumatano na
Dkt. Abdallah Possi ( Mb), Naibu Waziri, Ofisi
ya Waziri, wakati alipokuwa akichangia
majadiliano kuhusu mada ya
uondoaji wa umaskini na
kukosekana kwa usawa kwa watu wote wenye ulemavu. Mhe Possi
alikuwa mmoja wa wanajopo watano, walioongoza majadiliano kuhusu mada hiyo katika siku ya
pili ya mkutano wa tisa wa Mkataba wa
Watu Wenye Ulemavu unaoendelea hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.
Katika mchango wake, Naibu Waziri amesisitiza kwamba suala la upatikanajji wa vifaa saidizi kwa watu wenye ulemavu ni muhimu sana kwa kile alichosema ukosefu wa vifaa hivyo
ni moja wa changamoto kubwa kwa
watu wenye ulemavu.
Akatoa wito kwa
serikali, jumuiya ya kimataifa na asasi
za kiraia kuangalia ni kwa namna
gani katika wa umoja wao wanaweza
kushirikiana ili kukabili changamoto hiyo ya upatikanaji wa vifaa saidizi wa watu wenye ulamavu.
Mhe Possi anayeongoza ujumbe wa
Tanzania katika mkutano huu, pamoja na kuzungumza uhaba wa vifaa saidizi pia amezungumzia kwa
uzito wa aina yake kuhusu pamoja na mambo megine fursa ya upatikanaji wa
ajira kwa watu wenye ulemavu, unyanyapaji na mitizamo hasi dhidi ya watu wenye ulemavu.
Akasema
mitizamo hasi dhidi ya watu wenye ulemavu, ubaguzi na uyanyapaji umekuwa
kikwazo kikubwa katika siyo tu,
utekelezaji wa sera na mipango ikiwamo ya
fursa za ajira kwa walemavu, bali pia katika kufungua fikra na
mitizamo mipana na jumuishi kuhusu watu wenye ulemavu.
Aidha
Mhe. Naibu Waziri amerejea kauli
yake kwamba inakuwa vigumu
kutenganisha ulemavu na umaskini kwa
kile anachosema vinakwenda pamoja.
Akasisitiza ili watu wenye ulemavu
waweze kushiriki katika utekelezaji wa Agenda 2030, kujipatia fursa za ajira
kama ilivyo kwa watu wengine pamoja
na kuondokana na umaskini, jamii inao
wajibu mkubwa wa kutoa ushirikiano kuacha kuwabagua, kutowanyanyapa na kubwa zaidi kwa watendaji na wenye mamlaka serikali
kuandaa na kutekeleza mipango ambayo
ni jumuishi na yenye kuzigatia maslahi , mahitaji na
mazingira halisi ya watu wenye ulemavu.
Hoja ya vifaa saidizi kwa watu wenye ulemavu
iliungwa mkono na wanajopo wengine
kwa kile walichoeleza kwamba ni muhimu sana katika kuwafanya watu wenye ulemavu kuwa huru na
kuondokana na utegemezi.
Wanajopo hao mbali ya Dkt. Possi
walikuwa ni Bi. Asa Regner,
Waziri wa Waziri wa Watoto, Wazee na Usawa wa Jinsia kutoka Sweden, Bw. Joelson Dias ambaye ni Mwanasheria na Mjumbe wa Kamati ya Haki za watu wenye ulemavu kuotka
Brazil, Bi, Silvia Quam kutoka Guatemala
na Bi Emi Aizawa, kutoka Japan.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269