.

KATIBU MKUU RWEGASIRA AWAVISHA VYEO VYA MRAKIBU MSAIDIZI WAHITIMU 98 WA JESHI LA MAGEREZA, JIJINI DAR ES SALAAM

Jun 14, 2016

Katibu Mkuu  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (aliyevaa kiraia), akiongozana na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, CGP John Minja (katikati) na Mkuu wa Chuo cha Magereza Ukonga, ACP Erasmus Kundy (kulia), kuelekea katika viwanja vya Chuo cha Polisi Ukonga kwa ajili ya hafla ya kufunga mafunzo ya uongozi ngazi ya juu na kuwatunuku maafisa magereza 98 Cheo cha Mrakibu Msaidizi. Hafla hiyo ilifanyika Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, akikagua gwaride wakati wa kufunga mafunzo ya uongozi ngazi ya juu na kuwatunuku Maafisa Magereza 98 Cheo cha Mrakibu Msaidizi. Hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.
Gwaride la heshima likipita mbele ya Mgeni Rasmi, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (hayupo pichani), wakati wa kufunga mafunzo ya uongozi ngazi ya juu na kuwatunuku Maafisa Magereza 98 Cheo cha Mrakibu Msaidizi. Hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kulia), akimvisha cheo cha Mrakibu Msaidizi, mmoja wa wahitimu 98 wa Jeshi la Magereza, wakati wa kufunga mafunzo ya uongozi ngazi ya juu na kuwatunuku Maafisa Magereza 98 Cheo cha Mrakibu Msaidizi. Hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, CGP John Minja, akihutubia wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya uongozi ngazi ya juu na kuwatunuku Wahitimu 98 wa Cheo cha Mrakibu Msaidizi. Hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, akizungumza wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya uongozi ngazi ya juu na kuwatunuku Maafisa Magereza 98 Cheo cha Mrakibu Msaidizi. Katika hotuba yake Katibu Mkuu aliwaasa wahitimu hao wakaitumie taaluma walioipata chuoni hapo kwenda kuwahudumia Watanzania kwa uadilifu. Hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wahitimu wa mafunzo ya Uongozi wa Ngazi za juu wa Jeshi la Magereza, wakimsikiliza Mgeni Rasmi, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (hayupo pichani), wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya uongozi ngazi ya juu na kuwatunuku Maafisa Magereza 98 Cheo cha Mrakibu Msaidizi. Hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, akiwapungia mikono wageni waalikwa mara baada ya kufunga rasmi mafunzo ya uongozi wa ngazi ya juu wa Jeshi la Magereza na kuwatunuku Wahitimu 98 wa Cheo cha Mrakibu Msaidizi. Hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam. 

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª