.

BARAZA LA WAFANYAKAZI MUHIMBILI LAFANYA KIKAO CHAKE CHA 16, WAJUMBE WATAKIWA KUWA MFANO KWA WATUMISHI WENGINE.

Jul 1, 2016

NA NEEMA MWANGOMO
Baraza la wafanyakazi la Hospitali ya Taifa Muhimbili ,  limefanya kikao chake cha 16 ambapo pamoja na mambo mengine Agenda mbalimbali zimewasilishwa na kujadiliwa katika kikao hicho.
Kikao hicho kimefanyika  katika Ukumbi wa NACTE Mikocheni Jijini Dar es salaam.
Katika kikao hicho,  Baraza  limepokea na kujadili Bajeti ya mwaka wa fedha 2016/2017,limepokea na kujadili mpango kazi kwa mwaka wa fedha 2016/2017, limepokea na kujadili mipango ya manunuzi  katika kipindi cha mwaka wa fedha 2016/2017 .
Awali kabla ya kuwasilishwa kwa ajenda hizo,  mtoa mada kutoka Tume ya Usuluhishi na Uamuzi-CMA- Andrew Mwalwisi amewataka wajumbe wa baraza  kutimiza wajibu wao na kuitendea  taasisi yaliyo mema kwa kua mfano kwa watumishi wengine.
“Mtimize wajibu wenu  ipasavyo na kila mmoja  awe mshauri mzuri  katika kitengo anachokiongoza kwani kwa kufanya hivyo hata wetendaji wa chini wataiga mfano wenu” amesema Mwalwisi.
Pia  amewasisitiza wajumbe hao kutofanya kazi kwa mazoea na kufuata maadili ya Utumishi wa Umma na kuongeza kuwa kukosa maadili ya utumishi wa Umma kunaweza vunja amani ya baraza.

Kwa upande wake Katibu wa TUGHE Mkoa , Gaudence Kadyango amelitaka Baraza hilo kutambua kuwa majadiliano ni sehemu ya kazi hivyo pande zote mbili  zinatakiwa kuwa na busara kwa kila mmoja kusikiliza hoja ya mwezie.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª