Breaking News

Your Ad Spot

Jul 12, 2016

DK.SHEIN AZUNGUMZA NA WAZEE MJINI UNGUJA


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake kwa wazee waliotimiza umri wa miaka 70 katika hafla maalum ya ilyofanyika kumpongeza yeye Rais iliyofanywa na Wazee hao katiika Viwanja vya makaazi ya Wazee Sebleni Mjini Unguja leo Juluai 12, 2016. (PICHA NA IKULU YA ZANZIBAR)


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na baadhi ya Wazee ambao wametimiza miaka 70 ambao wanapokea mafao maalum ya uzeeni yaliyoidhinishwa na Rais wakati alipofika katika Viwanja vya Wazee Sebleni kwa ajili ya kumshukuru na Kumpongeza
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mzee Bi Mtumwa Ali Khamis ambae alishiriki katika mchezo wa kuigiza  wakati wa Shukrani na Pongezi maalum kwa Rais wa Zanzibar zilizotolewa na Wazee waliotimiza umri wa miaka 70 katika hafla iliyofanyika leo viwanja vya makaazi ya Wazee Sebleni Mjini Unguja
Msoma utenzi Bw.Mohamed Abdalla Zungu kutoka Kijiji cha Uroa Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja akighani Utenzi wake wakati wa hafla ya Shukrani na Pongezi maalum kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein zilizotolewa leo na Wazee wanaopokea pencheni kwa kutimiza umri wa miaka 70 katika Viwanja vya makaazi ya Wazee Sebleni Mjini Unguja


Wazee wa Wilaya ya Kusini Unguja nao waliohudhuria katika hafla ya kumponheza na kumshukuru Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kwa kuwawezesha kupata mafao ya kufikia umri wa miaka 70 katika hafla iliyofanyika leo viwanja vya makaazi ya Wazee Sebleni Mjini Unguja

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages