Mkurugenzi
wa Shirika hilo, Mugisha Rutasitara, akitoa ufafanuzi juu ya zoezi la
Upimaji wa Afya bure pamoja na uchangiaji wa damu kwa hiari,
linalofanyika katika uwanja wa shule ya Msingi Mirongo Jijini Mwanza,
kuanzia leo hadi jumamosi Julai 16,2016.
Na BMG
Bernadino
Ivo Medaa, ambae ni Afisa Uhamasishaji Mpango wa Taifa wa damu salama
Kanda ya Ziwa, akitoa ufafanuzi juu ya namna zoezo la uchangiaji wa damu
kwa hiari linavyoendelea Kanda ya Ziwa.
Mmoja
wa wakazi wa Jiji la Mwanza waliojitokeza kupima afya pamoja na
kuchangia damu katika zoezi linalofanyika uwanja wa shule ya Msingi
Mirongo kuanzia leo hadi jumamosi.
Mmoja
wa wakazi wa Jiji la Mwanza waliojitokeza kupima afya pamoja na
kuchangia damu katika zoezi linalofanyika uwanja wa shule ya Msingi
Mirongo kuanzia leo hadi jumamosi.
Timu
ya Continental Decoder, wauzaji wa Ving'amuzi nchini wakiwa wamejipanga
kwa ajili ya kuwahudumia wateja wao. Continental Decoder ni miongoni
mwa waliofanikisha zoezi la upimaji wa afya bure pamoja na utoaji wa
damu kwa hiari ambalo linafanyika kuanzia leo hadi jumamosi katika
Uwanja wa Shule ya Msingi Mirongo Jijini Mwanza.
Wakazi
wa Jiji la Mwanza wamekuwa na mwamko mkubwa wa kupima afya zao hususani
kwa magonjwa yasioyopewa kipaumbele ambapo idadi ya watu imeongezeka
kutoka 60 kwa kipindi cha mwezi mmoja hadi kufikia 2000 kwa kipindi kama
hicho.
Idadi
hiyo ni kwa mjibu wa Shirika la Reach and Support All (SARA) la Jijini
Mwanza, ambalo linashughulika na masuala mbalimbali ya kijamii ikiwemo
afya, elimu pamoja na utatuzi wa migogoro ya kifamilia.
Pamoja
na ongezeko la idadi hiyo, Mkurugenzi wa Shirika hilo, Mugisha
Rutasitara, ametoa msisitizo zaidi kwa wananchi kuwa na desturi ya
kupima afya zao hususani kwa magojwa yasiyopewa kipaumbele ikiwemo
uzito, presha na kisukari ili kuepukana na madhara ya kiafya ikiwemo
vifo kabla ya wakati.
Rutasitara
ameyabainisha hayo hii leo, katika zoezi la upimaji wa afya bure kwa
wakazi wa Jiji la Mwanza ambapo ameongeza kwamba wananchi wengi wana
tabia ya kwenda hospitalini baada ya kuzidiwa magonjwa, jambo ambalo
husababisha uwezekano mdogo wa wao kupona kutokana na kuchelewa matibabu
na kwamba jitihana za shirika hilo ni kuhakikisha watanzania wote
wanakuwa na desturi ya kupima afya zao mara kwa mara ili kutambua afya
zao mapema.
Zoezi
la upimaji wa afya bure kwa wakazi wa Jiji la Mwanza, limeenda sambamba
na wananchi kuchangia damu kwa hiari ambapo, Bernadino Ivo Medaa, ambae
ni Afisa Uhamasishaji Mpango wa Taifa wa damu salama Kanda ya Ziwa,
amesema bado kuna changamoto kwa mwananchi mmoja mmoja kuchangia damu
ikilinganishwa na wale wanaokuwa katika taasisi za elimu pamoja na dini.
Baadhi
ya wananchi waliojitokeza kuchangia damu Jijini Mwanza, wamewatoa hofu
wale ambao hawana desturi hiyo kwani hakuna madhara yoyote ya kiafya kwa
mtu anaechangia damu huku pia wakiwakumbusha kuwa na desturi ya kupima
afya zao mara kwa mara.
Zoezi
la upimaji wa afya bure na uchangiaji wa damu kwa hiari Jijini Mwanza,
linanyika kwa siku tatu kuanzia leo ambapo Mashirika mbalimbali ikiwemo
The Dest and Chair Foundation, Continental Decoder, Mpango Taifa wa damu
salama Kanda ya Ziwa pamoja na Reach And Support All, yamesaidia
kufanikisha zoezi hilo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269