.

MSF YAKARIBISHA USITISHAJI VITA KATIKA MJI WA ALEPPO SYRIA

Aug 20, 2016

Jumuiya ya Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) imeunga mkono pendekezo la kusimamis
ha mapigano katika mji wa Aleppo huko Syria.
Pablo Marco, Mkurugenzi wa jumuiya hiyo katika eneo la Mashariki ya Kati amesema kuwa MSF inakaribisha hatua ya Russia ya kuunga mkono suala la kusimamisha vita kwa muda wa masaa 48 katika mji wa Aleppo nchini Syria. Marco ameongeza kuwa wakazi wa Aleppo wanahitajia sana amani na utulivu.
Mkurugenzi wa Jumuiya ya Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) amesema usitishaji vita kwa muda wa masaa 48 huko Aleppo utatoa fursa ya kupelekwa misaada katika mji huo na kuwaondoa raia waliojeruhiwa na wagonjwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Wizara ya Ulinzi ya Russia jana ilitangaza kuwa inaunga mkono pendekezo la Stephen de Mistura, Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Syria la kusimamisha mapigano huko Aleppo kwa muda wa saa 48.
Stephen de Mistura Mjumbe Maalumu wa UN kuhusu Syria
Wizara hiyo imesema pia kuwa Moscow ipo tayari kusaidia utekelezaji wa makubaliano hayo wiki ijayo.  Jeshi la Syria likisaidiwa na vikosi vya jeshi la anga la Russia tangu wiki mbili zilizopita lilianzisha oparesheni kubwa ya kijeshi kwa minajili ya kuwatimua magaidi katika mji wa Aleppo na hadi sasa magaidi wa Daesh  na wa makundi mengine ya kigaidi zaidi ya 1000 wameuliwa na wengine karibu 2500 kujeruhiwa.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช