Bw. Simon Kivamwo |
Waandishi
wa habariwakitoa damu ili kuwezesha matibabu ya Mwandishi wa habari
mkongwe hapa nchini Bw. Simon Kivamwo ambaye anapatiwa matibabu kwenye
hospitali ya Ocean Raod iliyoko jijini Dar es Salaam leo Agosti 30,
2016.
Kwa mujibu wa Mwandishi wa Habari anayeratibu zoezi hilo
Bw.Thompson, Kivamwo ambaye anaugua kwa muda mrefu sasa, amezidiwa na
maradhi leo hii na kupelekwa haraka kwenye hospitali hiyo ambapo madaktari
walihitaji kumuongezea damu.
Benjamin Thomspon ametoa mwito kwa
wanahabari na jamii kwa ujumla kujitokeza kumchangia damu mwandishi huyu ili kuokoa maisha yake. Sehemu ya kutolea damu ni Hospitali ya
Mnazi Mmoja, Kariakoo jijini Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269