Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia ya wakazi wa
Geita mjini mara baada ya kuwasili kutoka Kahama.
RAIS
John Pombe Magufuli, ameagiza masalia ya mawe yanayotokana na uchimbaji
dhahabu kwenye mgodi wa kuchimba dhahabu wa Geita Gold Mine, maarufu
kama "Magwangala", wapewe wananchi masikini.
Rais
alitoa agizo hilo wakati akihutubia mamia ya wakazi wa Geita mjini
wakati alipowasili mjini humo akitokea wilayani Kahama, katika ziara
yake aliyoianzia mkoani Dodoma.
"Natoa
wiki tatu, mchakato wa kuyagawa Magwangala uanze mara moja, naagiza
NEMC kwa kushirikiana na taasisi nyingine, waanze utaratibu wa kuyagawa
magwangala mara moja, na asije akajitokeza mtu kuzuia agizo langu," rais
alisema.
Rais
Magufuli alisema, Dhahabu ni ya watanzania, na kama isingekuwepo hao
wanaozuia wasingeweza kufanya hivyo, " Lakini nawaomba ndugu wananchi,
zoezi hilo litakapoanza, lianze kwa utaratibu bila ya kuleta madhara."
Rais alishauri.
Swala
la magwangala kugawiwa kwa wananchi limekuwa likileta mvutano mkubwa na
kwa kiasi fulani swala hilo lilitaka kuathiri kampeni za CCM mkoani
Geita hadi makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, alipowaahidi wananchi
kuwa serikali itahakikisha swala hilo linapatiwa ufumbuzi na serikali
kwa haraka iwezekanavyo.
Wananchi wakishangilia hotuba ya Rais.
Rais Magufui akiwapungia mkono wananchi wakati akiwasili Geita mjini. (PICHA NA IKULU)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269