Breaking News

Your Ad Spot

Aug 29, 2016

RAIS WA KENYA ATILIA MKAZO UMUHIMU WA KIKAO CHA TICAD

Rais wa Kenya amesema kuwa mkutano wa sita wa Kimataifa wa Maendeleo kati ya Afrika na Japan utastawisha uwezo wa kiuchumi wa bara la Afrika.

Rais Uhuru Kenyatta amesema kuimarishwa uhusiano wa kiuchumi na kibiashara na Tokyo katika fremu ya Mkutano wa Sita wa Pamoja kati ya Afrika na Japan chini ya anwani ya "Mkutano wa Kimataifa wa Maendeleo ya Afrika" kutaleta nguvu ya kiuchumi barani Afrika. 

Rais Kenyatta ameongeza  kuwa kushiriki vyema Japan katika sekta za kiuchumi barani Afrika kuna umuhimu na kwamba hatua hiyo italeta ustawi wa pande zote katika bara hilo.

Naye Shinzo Abe Waziri Mkuu wa Japan amesisitiza pambizoni mwa mkutano huo juu ya kuimarishwa uhusiano wa pande zote na nchi za Kiafrika. Kikao hicho cha Naironi ni mkutano wa kwanza wa kimataifa kuwahi kusimamiwa na Tokyo kwa ajili ya maendeleo ya Afrika katika muda wa miaka 20 iliyopita, ambao umefanyika nje ya Japan.


Kikao cha Sita cha   Pamoja kati ya Afrika na Japan chini ya anwani "Mkutano wa Kimataifa wa Maendeleo ya Afrika ambao ulianza huko Nairobi mji mkuu wa Kenya tangu Jumamosi iliyopita kwa kuhudhuriwa na viongozi wa kisiasa na shakhsia wa kiuchumi wa Kiafrika na wa Japan, ulimalizika jana. Mkutano wa Kwanza wa Kimataifa wa Maendeleo ya Afrika ulifanyika mwaka 1993 huko Tokyo Japan na kuanzia wakati huo Japan imekuwa ikiunga mkono kuimarishwa ushirikiano wa kiuchumi kati yake na Afrika ikiwa kama mshirika wa kistratejia wa bara hilo.

Viongozi wa kisiasa na kiuchumi wakiwa pamoja baada ya mkutano wa Ticad jijini Nairobi

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages