Breaking News

Your Ad Spot

Aug 25, 2016

SABABU ZA MPENDAZOE KUITOSA CHADEMA NA KURUDI CCM HIZI HAPA

Tarehe 23 July 2016 nilishiriki kwenye Mkutano Mkuu wa CCM. Kwenye mkutano huo nilipata nafasi ya kuzungumza na haya Ndiyo niliyoweza kuyasema Kwenye mkutano huo:

Nilieleza kwamba kwa muda mrefu Nilikuwa nimeamua kurudi CCM, siku hiyo ilikuwa ni siku ya kutangaza tu. Nilikuwa nimeamua kurudi CCM kwa sababu kuu zifuatazo. Kwanza ni hatua ambazo CCM ilikuwa imeanza kuzichukua kupitia Katibu Mkuu wake Kinana. Kinana alifanya ziara nchi nzima akiwaeleza na kuwataka wanachama wa CCM kubadilika. Akiwaeleza wapige vita ufisadi, CCM iisimamie serikali yake. Aliwataka mawaziri wafanyekazi Kwa bidii. Aliikosoa serikali. Alisikiliza kero za wananchi wa chini na akawasemea Kwenye serikali yao. Watanzania wakaanza kupata matumaini.

Wakati Kinana akiendelea na ziara, CDM na UKAWA walihubiri mabadiliko majukwaani na kuzungusha mikono Lakini miyoni mwao hawakuwa tayari kubadilika. CCM kubadilika na kukubalika na wananchi.

Jambo jingine , CDM na UKAWA walimpokea mgombea aliyekuwa ameondolewa Kwenye kura za maoni ndani ya CCM. Mgombea huyo aliondolewa kwa tuhuma za ufisadi. UKAWA wakamchukua. Mtakumbuka, CDM walizunguka nchi nzima na wakadai wanao ushahidi kwamba mgombea huyo ni fisadi. CCM walimuondoa wao wakampokea akawa mgombea urais. Wasambaa wanao msemo unaosema, "ukitaka kuepuka nzi tupa kibudu". CCM ilitupa kibudu kilichokuwa kinasababisha harufu mbaya.

Hatua hii ya CDM na UKAWA kukumbatia kibudu kimesababisha CDM na UKAWA kimepoteza ajenda ya kupinga ufisadi na sasa ipo harufu ya mzoga ndani ya CDM na UKAWA.
Sababu nyingine ni hatua ambazo JPM na serikali yake amechukua. JPM amechukua hatua madhubuti kupiga vita ufisadi, uzembe na ubadhirifu. JPM ameleta matumaini kwa watanzania.
JPM Kama Mwenyekiti wa CCM amesema ni kweli CCM ilikuwa imepoteza dira. Nilipokuwa CCM pia nilisema kwamba CCM ilikuwa imeyumba. Niliyoyapigia kelele kwa sasa tunaye mtanzania ambaye amejitoa kuyashughulikia.

Lakini, Nani asiyefahamu kwamba ndani ya CDM demokrasia imeminywa kuliko Kwenye vyama vingine vya siasa?
Hahitaji utaalamu mkubwa kuchunguza na kubaini kwamba maamuzi ya kumtoa Dk Slaa kuwa mgombea hayakuwa ya kidemokrasia na ya harufu ya rushwa?
Maamuzi ya kupata mgombea yalifanyika Kwenye chopa !?.
Hivi CDM na UKAWA wanapigania nini? Siyo demokrasia. Hapana.

Ni Kwa sababu hizi nimerudi CCM.

CHANZO: WANABIDII

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages