Breaking News

Your Ad Spot

Aug 21, 2016

SANTOS ACHAGULIWA TENA KUONGOZA CHAMA TAWALA ANGOLA

santo
Jose Eduardo dos Santos amekuwa madarakani kwa miaka 36
Rais wa Angola, Jose Eduardo dos Santos aliyeongoza kwa miaka 36 amechaguliwa tena kuwa kiongozi wa chama tawala cha MPLA.

Uchaguzi wa bunge unatarajiwa kufanywa mwaka ujao, na kiongozi wa chama kinachoshinda ndiye anayekuwa rais.
Rais dos Santos alisema awali mwaka huu, kwamba ataondoka madarakani mwaka wa 2018, lakini ameshawahi kutoa ahadi kama hizo kabla.

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 73, analaumiwa kuwa amekusanya madaraka mengi na mali, kwenye mikono ya familia yake na washirika wake wakubwa kisiasa. BBC

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages