Waziri
wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi
Akizungumza na Maafisa mipango miji jijini Dar es salaam. Kulia Mkurugenzi wa Nyumba wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Michael Mwalukasa.
WAZIRI wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amewataka watendaji wa wizara hiyo kuendelea kujenga nyumba za makazi za watumishi wa serikali mkoani Dodoma.
Akizungumza
na maafisa wamipango miji jijini Dar es salaam leo Waziri Lukuvi
amewataka watendaji hao kuweza kujipanga kujenga nyumba za makazi za
watumishi wa Serikali ilikuweza kuwahudumia watumishi hao wanaotarajia
kuhamia mjini Dodoma.
''Lengo
la kikao hiki ni kuwataka mjipange ili kuweza kujipanga ni namna gani
mtaweza kuhudumia watumishi wa serikali wakati wakiwa mjini
Dodoma''amesema Waziri Lukuvi.
Amesema
kuwa sambamba na wizara mbalimbali kuhamia katika jiji la Dodoma
amewataka watendaji hao kuweza kuboresha ramani ya mipango miji
ilikuonesha namna gani mji unavyotakiwa kukaa ikiwemo kuboresha
miundombinu ya majengo .
''Tumeshamaliza mastar Plan tangu mwaka 2010 ya Dodoma kwani maeneo mengi yakuishi yameshaainishwa nilazima maafisa mipango kufanya biashara ikiwemo viwanja vyandege.
Nae
Katibu wa Wizara hiyo, Michaeli Mwalukasa amesema kuwa serikali
inaandaa sera ya nyumba ikiwemo muswada wa uendelezaji miliki katika
miji mbalimbali hapa nchini.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269