.

WAZIRI SIMBACHAWENE ASISITIZA KWAMBA SERIKALI ITATEKELZA AHADI ZAKE

Aug 27, 2016

WAZIRI SIMBACHAWENE

Na Sheila Simba, MAELEZO
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawene amesema kuwa Rais Magufuli amedhamiria kuwatumikia wananchi na kuhakikisha maendeleo yapatikani kwa Watanzania wote.

Akizungumza katika kipindi kipya cha “TUNATEKELEZA” kinachoandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO na TBC1 Waziri Simbachawene alisema kuwa serikali ipo kwa ajili ya kufanya kazi ya kuwatumikia wananchi katika kila sekta ili kutatua changamoto zinazowakabili.

“Kupitia falsafa yetu ya hapa kazi tu tutahakikisha tunawaletea wananchi maendeleo kutokana na ahadi zilizoaidiwa kutoka katika ilani 2015-2020 ya Chama Cha Mapinduzi kilicho na serikali.”

Alisisitiza kuwa Rais Magufuli ameamua kuleta mabadiliko ya kweli hapa nchini ambayo yanalenga kuwabana wabadhirifu wa mali za umma na kurejesha kurejesha nidhamu ya kazini jambo ambalo limeanza kuonekana katika Ofisi mbalimbali za umma.

Waziri huyo amewahakikishia wananchi kuwa ahadi za maendeleo zilizotolewa na Serikali ya awamu ya tano zitatekelezwa kama ilivyopangwa kwani wanayo dhamira ya kweli ya kuwatumikia wananchi.

Alisema kuwa suala la kusimamiana kazini ni la kawaida na ni wajibu wa kila mtumishi hakikishe anatimiza wajibu wake katika nafasi aliyopewa ili aweze kutekeleza majukumu yake kwa ajili ya kurahisisha utendaji kazi wa serikali kwa kuweka uzalendo mbele.

Aliongeza kuwa ari na nidhamu ya utendaji kazi mikoani imebadilika na watu wanafanya kazi kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora,kwani baadhi ya watumishi wa Halmashauri walikuwa wanafanya kazi kwa mazoea.

Kuhusu watumishi hewa alisema kuwa serikali imeondoa watumishi 12,000 waliokua wananchukua mishahara bila kufanya kazi na kuomba wananchi kuunga mkono juhudi za serikali katika hatua wanazochukua.

“upangaji mzuri wa watumishi kwenye maeneo ya utoaji huduma kwa wananchi kwa maana ya Halmashauri utakuwa umekaa vizuri kwa asalimia kubwa hata kwa kuwapanga vizuri bila wafanyakazi hewa kuwepo”alifafanua Waziri Simbachawene

Alisema kuwa suala la wataalamu wa fani mbalimbali kupendelea kubaki mijini ni tabia na kukosa uzalendo kwani baadhi ya watumishi wanaopagiwa mikoani hawaripoti kutokana na mazingira jambo ambalo sio sahihi.

“hata huku mijini wanakokimbilia hakuna nyumba za watumishi basi imekuwa ni tabia tu ya watu kukosa uzalendo”alisema Simbachawene.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช