Breaking News

Your Ad Spot

Sep 5, 2016

BALOZI WILSON MASILINGI AONGEA NA WATANZANIA NC AWAASA UPENDO NA KUSHIKAMANA, WAMUAHIDI KUCHANGIA MADAWAT


Gloria Alex Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Watanzania North Carolina (UTNC) akiongea machache ya kumshukuru Mhe. Balozi Wilson Masilingi na baadae kumkaribisha kuongea na Wtanzania wa Carolina ya kaskazini siku ya Jumamosi Septemba 3, 2016 katika ukumbi uliopo hoteli ya Comfort Suites jijini Durham, North Carolina.
 Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Wilson Masilingi akiongea na Watanzania wa North Carolina siku ya Jumamosi Septemba 3, 2016 katika ukumbi wa hoteli ya Comfort Suites jijini Durham, North Carolina. Katika hotuba ya Mhe. Balozi Wilson Masilingi aliwaasa wanaUTNC kupendana na kushikamana na kusaidiana kuonyeshana njia za mafanikio badala ya kukalia majungu na kuchukia maendeleo ya mwenzako. Mwenzako anapofanya vizuri mpe sifa yake na muulize amefikaje hapo na yeye akusaidie ufikie hapo alipo.

Mhe. Balozi Wilson Masilingi aliwasisitizia Watanzania wa North Carolina wajenge desturi ya kuwekeza nyumbani na kuwaelekeza jinsi ya kufungua akanti za akiba kwenye benki za Tanzania ili ziweze kuwasaidia kwa siku za usoni kwa maendeleo yao nchi Tanzania kwa kuwezesha kununua kiwanja na hatimae kujijengea kibanda.

Mhe. Wilson Masilingi aliwasisitizia wanajumuiya hao kutafuta wawekezaji watakaoingia nao ubia na wahakikishe hawaingii mikataba na watu wa kati na yeye kwa kutumia ofisi ya Ubalozi ameahidi kuwasaidia ili kuwaondolea wawekezaji usumbufu unaoweza kujitokeza pindi wanapoamua kujifanyia wenyewe kwani wanaweza kuangukia kwenye mikono isioitakia mema Tanzania.

Mhe. Balozi aliwaachia uongozi wa Jumuiya hiyo ya Umoja wa Watanzania North Carolina wito wa kuunga mkono juhudi za Rais John Pombe Magufuli za kuchangia madawati na Mwenyekiti mstaafu awamu ya tatu, Bwn. Geofrey Lepana aliitikia wito huo kwa kuchanga dola 80 pesa taslimu papo hapo kwa Mhe. Balozi Wilson Masilingi na yeye kuukabidhi mchango huo kwa mwenyekiti wa jumuiya ya Umoja wa Watanzania North Carolina, Bi. Gloria Alex na yeye kuahidi kwa niaba ya uongozi wake kuufanyia kazi wito huo.
Afisa Ubalozi Bwn. Abbas Missana akifuatilia hotuba ya Mhe. Balozi Wilson Masilingi.
Bwn. Nassoro Basalama, mwenyekiti mstaafu akidadavua historia ya jumuiya hiyo kwa Mhe. Balozi Wilson Masilingi.
 Mwenyekiti mstaafu Geofrey Lepana akipena mikono na Mhe. Balozi Wilson Masilingi mara baada ya kuchangia dola 80 kwa ajili ya madawati.
Mhe. Balozi Wilson Masilingi akimkabidhi mchango huo mwenyekiti wa Umoja wa Watanzania North Carolina, Bi. Gloria Alex.
Mweka hazina wa Jumuiya Pandwe Kalala ambaye ndie aliyekua mshereheshaji wa mkutano huo wa Watanzania wa North Carolina na Balozi.
 
Dr. Mishael Muze aliyewahi kushika nyazifa mbalimbali serikalini ikiwemo kamishna wa elimu akiunga mkono juhudi za Rais Magufuli za kuchangia madawati.
 Wanajumuiya wakifuatilia hotuba ya Mhe. Balozi Wilson Masingi.
Viongozi wa Jumuiya ya Umoja wa Watanzania North Carolina wakiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Balozi Wilson Masilingi pamoja na mkewe Marystela Masilingi,

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages