Na Daudi Manongi, MAELEZO
Shirika la Maji Safi na Maji taka Dar es Salaam (DAWASCO) limetangaza kuzima mtambo wa kuzalisha Maji wa Ruvu Juu kwa wakazi wa Dar es salaam na Mji wa Kibaha Pwani kwa saa 14 kesho Ijumaa kuanzia saa tatu asubuhi mpaka saa tano usiku.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya Habari na ofisi ya uhusiano ya shirika hilo leo jijini Dar es Salaam inaeleza kuwa sababu kuu ya kuzimwa kwa mtambo huo ni kuruhusu usafishaji wa bomba jipya na kufanya majaribio ya sehemu ya mtambo mpya wa Maji wa Ruvu juu.
Pia zoezi hili linahashiria hatua za mwisho za mtambo huo kukamilika na kuanza kutumika ili kuondoa tatizo la upatikanaji wa huduma ya Maji katika maeneo yanayohudumiwa na mtambo huo.
Maeneo ambayo yatakosa maji ni Mlandizi Mjini , Ruvu darajani, Vikuruti, Disunyara, Kilangalanga, Janga, Mbagala, Visiga, Lulinzi, Kibamba, Kibamba njia panda, Shule kibwegere, Mloganzira, Kwembe, Kibamba hospital, Kwa mkinga, Luguruni ,Maili 35, Zogowale, Misugusu,Tanita, Kibondeni, Kwa mathias, Nyumbu, Msangani, Kwa mbonde, Picha ya Ndege, Sofu na Gogoni.
Pia zoezi hili linahashiria hatua za mwisho za mtambo huo kukamilika na kuanza kutumika ili kuondoa tatizo la upatikanaji wa huduma ya Maji katika maeneo yanayohudumiwa na mtambo huo. Aidha Shirika linatoa ushauri kwa wananchi kuhifadhi maji na kuyatumia kwa matumizi ya lazima.
Your Ad Spot
Sep 1, 2016
Home
Unlabelled
MTAMBO WA MAJI WA RUVU JUU KUZIMWA KWA SAA 14 KESHO
MTAMBO WA MAJI WA RUVU JUU KUZIMWA KWA SAA 14 KESHO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269