Breaking News

Your Ad Spot

Sep 27, 2016

RAIS DK MAGUFULI KUZINDUA KESHO NDEGE MPYA ZA ATC

Na Lilian Lundo-MAELEZO
Rais Dk. John Magufuli kesho anatarajiwa kuzindua ndege mbili za Shirika la Ndege la Tanzania (ATC) zilizonunuliwa kwa kutumia kodi za wananchi.

Uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal 1).

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu (Uchukuzi), Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dk. Leonard Chamuriho leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa ndege hizo.

Dk. Chamuriho alisema kuwa ndege ya kwanza iliwasili nchini tarehe 20/09/2016 na ndege ya pili ilitarajiwa kuwasili nchini leo tarehe 27/09/2016 kuanzia saa 6:00 mchana.

Vile vile Katibu Mkuu huyo alisema kuwa ndege hizo zimenunuliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuhudumia wananchi wa ndani ya nchiya Tanzania na nchi jirani.

“Ndege hizo aina ya Dash 8 Q400 zimetengenezwa na kiwanda cha Bombadier nchini Canada ambapo kila moja ina uwezo wa kubeba abiria 76 na zitatumika katika kuhudumia soko la ndaniya Tanzania na nchi jirani,” alifafanua Dkt. Chamuriho.

Aidha, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inawakaribisha wananchi wote kushuhudia uzinduzi wa ndege hizo unaotarajiwa kuanza saa mbili kamili (2:00) asubuhi.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages