Breaking News

Your Ad Spot

Sep 7, 2016

SIMBA SC NA RUVU SHOOTING KUCHEZWA UWANJA WA UHURU ‘SHAMBA LA BIBI’

Mashabiki wakishangilia mara baada ya timu yao Simba kusawazisha kwa 1-1 katika Mchezo uliochezwa Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)


BAO la kipindi cha pili la mshambuliaji Mrundi, Laudit Mavugo limeipa Simba SC ushindi wa 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo.
Mavugo alifunga bao hilo lililowaamsha vitini mashabiki wa Simba SC Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam dakika ya tatu tu baada ya kuanza kipindi cha pili, akimalizia pasi ya Ibrahim Hajib.
Katika mchezo huo uliokuwa mkali na wa kusisimua, hadi mapumziko timu hizo zilikuwa zimefungana bao 1-1, Ruvu wakitangulia kabla ya Simba kusawazisha.

























Ruvu walianza kupata bao lililofungwa na  Abulrahman Mussa dakika ya saba akimalizia pasi ya Fully Maganga, kabla ya Simba SC kusawazisha kupitia kwa Ibrahim Hajib aliyemalizia krosi ya Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ dakika ya 11.Katika kipindi hicho kila timu iliweza kufanya mashambulizi
makali, huku Simba kupitia mchezaji Laudit Mavugo, akikosa nafasi tatu za wazi, katika dakika 19, 23 na 37 kwa kutokuwa makini.  Hajib naye akapoteza nafasi dakika ya saba na Kichuya dakika ya
21, kwa upande wa Ruvu Said Wigenge, akiwa yeye na kipa Vincent Angban alipiga shuti kali juu ya lango dakika ya 25.Kiungo wa Ndanda, Jabir Aziz alitolewa kwa kadi nyekundu nyekundu
dakika ya 79 baada ya kumchezea rafu kiungo wa Simba SC, Muzamil
Yassin. Kwa matokeo hayo, Simba SC inafikisha Ndanda FC pointi saba baada ya kucheza mechi tatu, awali ikishinda 3-1 dhidi ya Ndanda FC na baadaye kulazimishwa sare ya 0-0 na JKT Ruvu.Michezo mingine ya Ligi Kuu leo, Yanga SC imelazimishwa sare ya 0-0 na Ndanda FC Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara, wakati bao pelee la Muivory Coast, Kipre Balou limeipa Azam FC ushindi wa 1-0
dhidi ya wenyeji, Prisons Uwanja wa Sokoine, Mbeya.  Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Vincent Angban, Malika Ndeule, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Novaty Lufunga, Method Mwanjali, Jonas Mkude, Shiza Kichuya/Jamal Mnyate dk80, Said Ndemla/Muzamil Yassin dk71, Laudit Mavugo/Frederick Blagnon dk64, Ibrahim Hajib na Mwinyi Kazimoto. Ruvu Shooting: Abdallah Rashid, Damas Makwaya, Mau Bofu, Frank
Msese, Shaibu Nayopa, Jabir Aziz, Abulrahman Mussa/Baraka Mtuwi dk51, Shaaban Kisiga, Said Dilunga, Fully Maganga na Claide Wigengea

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages