Breaking News

Your Ad Spot

Sep 30, 2016

TANESCO YAFANYA KIKAO CHA UJIRANI MWEMA NA VIONGOZI WA JAMII INAYOZUNGUKA VITUO VYA KUFUA UMEME WA GESI VYA KINYEREZI JIJINI DAR ES SALAAM

 Meneja wa Kituo cha kufua umeme kinyerezi I, Mhandisi Lucas Busunge, akifungua kikao cha ujirani mwema kati ya TANESCO, TPDC na viongozi wa jamii inayozunguka Vituo vya kufua umeme wa Gesi vya Kineterezi jijini Dar es Salaam Septemba 30, 2016.
 Mkuu wa Kitengo cha Usalama, TANESCO Makao makuu, Misana Gamba

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
SHIRIKA la Umeme nchini TANESCO na viongozi wa dini, vyombo vya dola na viongozi wa Serikali za Mitaa sita inayozungu vituo vya kufua umeme wa Gesi asili vya Kinyerezi jijini Dar es Salaam, wamekubaliana kuweka mikakati ya pamoja kuhakikisha jamii inashiriki katika ulinzi wa miundombinu ya umeme.
Makubaliano hayo yamefikiwa leo Septemba 30, 2016, kwenye kikao cha ujirani mwema kati ya TANESCO, TPDC, viongozi wa dini, viongozi wa serikali za mitaa na vyombo vya dola ili kujadili namna bora ya kulinda miundombinu ya umeme kwenye vituo hivyo.
“Umeme wa Gesi ni umeme salama kabisa, hata hivyo ni wajibu wetu kushirikiana pamoja kuhakikisha miundombinu ya umeme huu wa Gesi inatunzwa na kulindwa,”, Meneja wa Kituo cha Umeme Kinyerezi I, Mhandisi Lucas Busunge alianza kwa kusema wakati akiwakaribisha wajumbe kwenye kikao hicho.
Tumeona tuitane hapa leo ili tujadiliane pamoja namna bora ya kuhakikisha umeme huu utokanao na Gesi ambao Serikali imeiingia gharama kubwa, miundombinu yake inalindwa na nyinyi viongozi mnao wajibu mkubwa wa kuwafikishia ujumbe wananchi wanaoishi maeneo yanayozunguka mitambo hii. Alisema Mhandisi Busunge.
Akitoa mada juu ya Mambo yanayoweza kusababisha uharibifu wa miundombinu ya umeme wa Gesi na hasara inayoweza kulikumba taifa na jamii kwa ujumla, Mkuu wa Usalama wa TANESCO makao makuu, Misana Gamba alisema, “Lazima tutambue kuwa Serikali imewekeza fedha nyingi katika ujenzi wa vituo hivi na fedha hizi ni za walipa kodi wa Tanzania, kwa hivyo ni wajibu wetu sote na sio TANESCO pekee kuhakikisha tunalinda miundombinu hii kwa manufaa ya sasa na vizazi vijavyo,” alisema Gamba
Akifafanua zaidi, Mkuu huyo wa usalama alibainisha mambo ambayo jamii inapaswa kuelewa kuwa ni hatari dhidi ya miundombinu ya umeme ambayo ni pamoja na kuwasha moto, kulima au kuchimba mchanga, mmomonyoko wa udongo, wezi wa vyuma, uvuvi haramu, kujenga, kufanya biashara au kuendesha magari makubwa sehemu ambayo miundombinu hiyo ya umeme wa Gesi inapita.
Mkuu huyo wa usalama wa TANESCO alisema, hatari inayoweza kutokea endapo mambo hayo yatafanywa ni pamoja na kurudisha nyuma jiyihada za Serikali katika kuwaletea umeme wananchi, lakini pia hatari ya kulipuka kwa mitambo hiyo ambapo madhama makubwa yanaweza kuwakumba wananchi.
Akichangia kwenye mazungumzo hayo, Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji, ambaye ndiye alikuwa muendesha kikao, alisema, Shirika la Umeme Tanzania, TANESCO, imekuwa ikitoa elimu kwa umma juu ya umuhimu wa kutunza miundombinu ya umeme kwa faida ya Watanzania wote, na hatua ya kikao hicho ni mwendelezo wa utoaji elimu na kuwataka viongozi hao kuwa mabalozi katika maeneo yao, kwenye nyumba za ibada, ili kusudi wananchi wengi waelewe umuhimu wa kuunza miundombinu ya umeme ambayo kimsingi ni mali ya Watanzania wote.
Naye afisa mwandamizi wa usalama Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini, (TPDC), Elias Muganda, alitahadharisha juu ya shughuli za kiuchumi kwenye eneo linakopita bomba la Gesi na ksuema hiyo ni hatari. “Kwa sasa kuna mabomba mawili yenye Gesi tayari, ambayo yako umbali wa mita 2 kwenda chini, yakipata mgandamizo unaosababishwa na magari makubwa kupita juu yake inaweza kupelekea leakge na kusababisha Gesi kuvuja na matokeo yake kila mtu anayajua ni moto.” Alifafanua
Akatoalea mfano wa mabomba yaitwayo Carthodic Protection, ambayo huzuia kutu, lakini tayari kuna watu wanang’oa vyuma hivyo na hii inaweza kusababisha kutu na mabomba kutoboka,alitahadharisha, Muganda.
Wakichangia mazungumzo hayo, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kanga, Shamte Mlanzi Mkali, alitoa wito kwa viongozi wenzake wa Mitaa, kila wanapokutana kwenye vikao, moja ya ajenda ya kuzungumza ni pamoja na usalama wa mitambo ya Gesi.
Hata hivyo viongozi wengi walionyesha umuhimu wa TANESCO kutoa ajira kwa vijana waishio maeneo ya jirani na mradi ili waweze kuona manufaa ya moja kwa moja ya ujio wa mradi huo.
Mambo yaliyoazimiwa kwenye kikao hicho ni pamoja na ulinzi wa miundombinu ya Gesi iwe ni moja ya ajenda za vikao vya Serikali za Mitaa, na iwe marufuku kwa mtu kupita au kukatiza eneo la Mitambo bila ya kibali maalum, uwepo utaratibu wa kuwaalika viongozi wa TANESCO/TPDC kwenye vikao vya Serikali za Mitaa kama itahitajika.
Maazimio mengine ya kikao hicho kilichomuhusisha pia Mkuu wa upelelezi wa Kituo cha Sitakishari-Ukonga,  SSP, Hassan Okello, ni pamoja na kampuni za ulinzi kwenye eneo la mitambo zijulikane kwa viongozi wa Serikali za mitaa yote inayozunguka eneo la mradi.
Mitaa iliyoshiriki kwenye kikao hicho ni pamona na Mtaa wa Kanga, Kibaga, Kinyerezi, Kichangani, na Kifura.

 Mhandisi Busunge
 Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji (aliyesimama), akizungumzia umuhimu wa viongozi wa mitaa kushirikiana na TANESCO katika kuelimisha umma, kutunza miundombinu ya umeme
 Afisa Usalama wa TANESCO makao makuu, Fidelis Almasi, akielezea namna viongozi wanavyoweza kushiriki katika kuelimisha wananchi umuhimu wa kutunza miundombinu ya umeme na athari za zitokanazo na uharibifu wa miundombinu hiyo kwa jamii na serikali
 Mkuu wa upelelezi, Kituo cha polisi Sitakishari-Ukonga, MrakibuMsaidizi wa Polisi, (ASP), Hassan Okello, akiwatoa hofu viongzoi hao kuhusu kutunza siri wanapotoa taarifa za wahalifu na uhalifu na kwamba yeye binafsi yuko tayari siku zote kuhakikisha usalama kwenye eneo hilo unazingatiwa
 Afisa Usalama Mwandamizi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini, (TPDC), Eliasi Muganda, amesema, mabomba mawili ya gesi tayari yana gesi na yako umbali wa kina cha mita 2 kutoka uso wa ardji na hivyo hayahitaji mgandamizo kutoka juu kwani ni hatari yanaeza kupata nyufa na kuvujisha Gesi

 Afisa Elimu wa Kata ya Kinyerezi, Mwalimu Mercy Mtei, (kulia), yeye amesema, atawashirikisha walimu na wanafunzi kueneza ujumbe kwenye jamii
 Sheikh Juma Swaleh wa Msikiti wa Othman Bin-Afan wa Kinyerezi
 Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kichangani, Niyukuli Leonard (kulia)
 Mchungaji Jacob Msami,  akizungumza
 Ustaadhi Ally akizungumza
 Mchungaji Ariel Mungereja wa Kanisa la EAGT, Kinyerezi
 Afisa Usalama wa Kituo cha Kinyerezi I, Furaha Munisi, akifafanua mambo mbalimbali ya kiusalama ambayo viongozi hao wanapaswa kuyachukua na kuwaelimisha wananchi
Picha ya pamoja baada ya kikao

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages