Breaking News

Your Ad Spot

Sep 8, 2016

THE POOL OF SILOAM CHURCH: SIYO KUPATWA KWA JUA, NI 'JUA LA HAKI'

Na Mwandishi Maalum
Tukio la kupatwa kwa jua lililotarajiwa na Dunia na kujiri katika mji mdogo wa Rujewa, Mbalali mkoani Mbeya nchini Tanzania, limeacha simulizi na dhana katika maono na imani mbalimbali zikiwemo za dini.

Mwandishi wa Kanisa la The Pool of Siloam, akieleza mtazamo wa kiimani wa Kanisa hilo, anaeleza kuwa Kanisa hilo linaliona tukio hilo kuwa si la kupatwa kwa jua, bali ni tukio lililogeuka kuwa la 'jua la haki' kuzuka na kufunika sehemu kubwa ya nchi kama ilivyoand 
ikwa katika Biblia, katika Malaki 4:1-4.


Anaeleza kuwa, watu wengi kutoka mataifa mbalimbali walilitarajia kwa hamu tukio hilo la kupatwa kwa jua lakini ikawa ni tofauti na matarajio hayo hata kwa wanasayansi na wanajimu kwa jinsi ilivyotokea jua la siku hiyo ya Septemba 1, 2016.


"Tukio la kuzuka kwa Jua la Haki kwa mara ya kwanza hapa Tanzania siku ya 12 adari, 3 (Novemba 16, 2014), ikiwa ni siku ya unyakuo wa Mjumbe wa Mapenzi ya Mungu, Eliya Ad2 (miaka 1000), Mungu wa Majeshi nyumbani kwake Bagamoyo mkoani Pwani ambapo Kanisa na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali walihudhuria", anaeleza mwandishi huyo.


Wakili wa Mungu Elisha Eliya (Ad2) miaka 1000, anayezungumziwa na mwandishi huyo, ndiye Kiongozi wa Kanisa hilo la The Pool of Siloam, ambalo katika miaka ya hivi karibuni limejizolea wafuasi wengi na kuwa na Makanisa yake katika maeneo mbalimbali hapa Tanzania.


Miongoni mwa taratibu za Kanisa hilo, kila muumini hutakiwa kuvaa mavazi nadhifu, maeupe anapokuwa katika shughuli mbalimbali za ibada kanisani au kwingineko.


Akieleza  zaidi mwandishi huyo anasema, "Pia kumekuwa na mwendelezo wa matukio hayo mara kwa mara tangu hiyo 12 Adari, 3 (Novemba, 16 2014) katika matukio mbali mbali yaliyohusisha shughuli za Kanisa la Siloamu", anaandika Mwandishi wa Kanisa hilo na kuongeza:-


"Kuzuka kwa jua hilo la Haki kulitokea katika matukio mbalimbali ikiwa ni pamoja na tukio la safari ya Kanisa kwenda jiji la Eliya (Kigoma) Januari 10, mwaka huu wa 2016,  lakini pia lilizuka siku Wakili wa Mungu alipofanya ziara katika mkoa wa Ararati (Kilimanjaro) ambapo aliwaambia wa mkoa huo kuwa aliyesikia Sauti ya Mungu, kizazi cha nne alizaliwa katika mkoa huo".


Anaeleza zaidi kwamba, Januari 26, mwaka huu(2016), akiwa katika mkoa wa Kigoma, ambao kwa mtazamo wa The Pool of Siloam ni jiji la Kigoma, Kiongozi wa Kanisa hilo, anayetajwa kwa hadhi ya Wakili wa Mungu Elisha Eliya miaka 1000(Ad2), aliwaambia wananchi wa mkoa huo wakati akihubiri, kuwa Kigoma ndio mahali ambapo sauti ya Mungu kizazi cha nne ilipitia hapo kwa kuwa ndipo alipoisikia Sauti ya Mungu akiwa hapo (Kigoma), mwaka 2003.


"Lakini pia katika ibada ya 23 shebati, 5 (Septemba 1, 2016) wakati akiahirisha ibada iliyoitwa ya Majibu Wakili wa Mungu Elisha Eliya, aliahirisha ibada hiyo kwa kusema yeye (Kiongozi wa Kanisa hilo), anakwenda kuangalia jua la haki na ndivyo ilivyotokea katika sehemu kubwa ya nchi", ameeleza mwandishi huyo.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages