Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Wilaya ya
Kati Unguja Mhe. Simai Mohammed Said, akizungumza na Vijana wa Kisiwa
cha Uzi wakati wa uzinduzi wa Baraza la Vijana la Shehia hiyo
lililozinduliwa na Waziri wa Kazi Vijana Uwezeshaji Wanawake na Watoto
Zanzibar Mhe Moldiline Castico katika viwanja vya Skuli ya Uzi.
Mc wa Mkutano huo wa Uzinduzi wa Baraza
la Vijana wa Shehia ya Kisiwa cha Uzi akisoma ratiba ya Uzinduzi huo
katika viwanja vya Skuli ya Uzi Wilaya ya Kati Unguja.
Mwanachama wa Baraza la Vijana la Shehia
ya Kisiwa cha Uzi Unguja Khadija Said akisoma Quran Tukufu kabla ya
Uzinduzi wa Baraza lao la Vijana la Shehia ya Uzi lililozinduliwa na
Waziri wa Kazi Vijana Uwezeshaji Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe,
Moldiline Castico.
Vijana wa Baraza la Vijana la Shehia ya
Kisiwa cha Uzi wakicheza maigizo ya kuhamasisha Vijana kujiunga na
Mabaraza ya Vijana kwa Maendeleo yao katika kujikwamua Kiuchumi.
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu akiwa na
Viongozi wa meza kuu wakifuatilia mchezo wa maigizo unaohamasisha Vijana
kujiunga na Mabaraza la Vijana katika Shehia zao.,
Mwanachama wa Baraza la Vijana Shehia ya
Kisiwa cha Uzi Salma Tunda akisoma risala yao mbele ya Mgeni rasmin
wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika viwanja vya skuli ya uzi.
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Shehia ya
Kisiwa cha Uzi Farashuu Mussa akitowa salamu za Baraza lake kwa mgeni
rasmin wakati wa uzinduzi huo.
Sheha wa Shehia ya Kisiwa cha Uzi Hamad Ramadhani akizungumza wakati wa uzinduzi huo wa Baraza la Vijana wa Kisiwa cha Uzi
Mkuu wa Wilaya ya Kati Unguja Mhe
Mashavu Sukwa akizungumza wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi wa Baraza la
Vijana Shehia ya Kisiwa cha Uzi Unguja na kuwataka Vijana kutumia
Mabaraza la Vijana kwa maendeleo yao katika kujitafutia Ajira.
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Wilaya yac
Kati Unguja Mhe Simai Mohammed Said akizungumza wakati wa hafla hiyo ya
Uzinduzi wa Baraza la Vijana la Shehia ya Kisiwa cha Uzi na kuichangia
shilingi laki mbili kwa kukuza mtaji wa Baraza hilo katika miradi yao
endelevu.
Waziri Moldiline Castico na viongozi wa
meza kuu wakimsikiliza Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu akitowa salamu za
Mbunge wa wake kwa Vijana wa Shehia ya Kisiwa cha Uzi wakati wa uzinduzi
huo uliofanyika katika viwanja vya Skuli ya Uzi.
Waziri Moldiline Castico akimkabidhi
fedha Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Shehia ya Kisiwa cha Uzi Farashuu
Mussa fedha zilizotolewa mchango na Mwakilishi wa Jimbo la hilo Mhe
Simai Mohammed Said ikiwa ni mchango wake kwa Baraza hilo la Vijana wa
Shehia ya Uzi.
Waziri wa Kazi Vijana Uwezeshaji
Maendeleo ya Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe Moldiline Castico
akiwahutubia Vijana wa Baraza la Shehia ya Kisiwa cha Uzi wakati wa
kulizindua Baraza hilo na kuwaasa Vijana kubuni miradi ya Maendeleo
yatakayowaletea Tija katika kukuza Uchumi wao kupitia Mabaraza hayo.
uzinduzi huo umefanyika katika viwanja vya Skuli ya Uzi.Wilaya ya Kati
Unguja Jimbo la Tunguu Zanzibar.
Vijana wa Baraza la Vijana Shehia ya
Kisiwa cha Uzi wakimsikiliza Mgeni rasmin wakati wa uzinduzi wa baraza
lao lililozinduliwa na Waziri wa Kazi Vijana Uwezeshaji Wanawake na
Watoto Zanzibar Mhe Moldiline Castico.
Sheha wa Shehia ya Uzi Ngambwa Amour Ali
akisoma dua baada ya hafla ya uzinduzi wa Baraza la Vijana la Shehia ya
Kisiwa cha Uzi, uliofanyika katika viwanja vya skuli ya Uzi Wilaya ya
Kati Unguja Jimbo la Tunguu Zanzibar.
Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot
Zanzinews.com.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269