Breaking News

Your Ad Spot

Sep 29, 2016

ZIMWI LA TEGETA ESCROW LAMTISHA PROFESA TIBAIJUKA, AKATAA KUPOKEA DOLA 300,000 BAADA YA KUPEWA TUZO YA KIMATAIFA

Mbunge wa Muleba Kusini, Prof. Anna
Tibaijuka akionyesha tuzo ya Kimataifaya
Maendeleo Endelevu ya Mwana Mfalme
Khalifa Bin Salman  Al Khalifa
aliyotunukiwa hivi karibuni
New York Marekani
Na Dotto Mwaibale
MBUNGE wa Muleba Kusini Profesa Anna Tibaijuka amekacha kupokea dola 300,000 alizopewa baada ya kutunukiwa tuzo ya  Maendeleo Endelevu aliyopewa na Umoja wa Mataifa (UN), kutokana na sakata la fedha za Escrow Tegeta.

Tuzo hiyo aliipokea Septemba 23 mwaka huu New York Marekani ambayo mfadhili wa tuzo hiyo ni wa waziri mkuu wa Bahrain mwana mfalume Khalifa bin Al Khalifa.

Akizungumza jana Dar es Salaam Profesa Tibaijuka alisema kwa sasa umoja wa mataifa umeingia katika awamu ya pili ya maendeleo, ambao umekuja kupisha yale malengo 17 ya mileniam ambayo yote yeye alikuwepo, hivyo aliokuwa wanatoa tuzo walinona kwa namna alivyoshiriki kwa kiasi kikubwa.

"Tuzo hizi si za kuomba, ni watu wanakaa na kupendekeza mtu wa kupewa, na hii ni mara ya pili, mara ya kwanza   nilipewa mwaka 2009 nchini Swideni," alisema na kuongeza.

"Tuzo zinatoka kwa niaba ya jamii inayotoka au kuitumikia na kufanya nayo kazi, hivyo wamatambua mchango wangu katika kuwatumikia wananchi wa Muleba," alisema.

Aidha Profesa tibaijuka alitaja sababu zilizpokekea yeye kutochua dola 300,000 za Marekeni za tuzo hiyo.

"Sikuichukua kwa sababu ya yaliyonikuta hapo mapema, kulikuwa na uwezekano wa kuichukua lakini nikasema kwa hali halisi ya nyumbani, hatuna sheria ya kupokea tuzo, michango na zawadi kwa hiyo mimi nikaicha mezani wao wafanye wanayotaka," alisema na kuongeza. 

"Unapoona mtu kama mimi nafanya kazi nakwenda kuchafulia kwenye kitu ambacho siusiki nacho, sasa Unapoipokea hapa utaonekana kama umevunja maadili au umejinufaisha kwa kuwa ndio mambo ya kwetu, hivyo nikawaachia," alisema.

Aliongeza kwa sasa umeshapeleka mswada binafsi bungeni wa kuweka sheria ya michango ili vitu vya hiari kama hivi vinapokuja katika jamii visimamiwe na si kupotoshwa kisiasa.

"Kwa maana jambo hili halina kificho, yaani huwezi kumzungumzia Anna Tibaijuka bila kutaja suala la Escro, hayo hayakwepeki kwa sababu yalitengenezwa yakawa hivyo, mtu asiyehusika anavalishwa joho lisilo muhusu.

"Lakini kwa sababu jamii haina uwezo wa kuchimba chini, unabaki kuwa uongo na kushindwa kujua ukweli umesimama wapi, lakini wao (UN) wanajua hii ni propanda la sivyo nisingesimama hapa na tuzo," alisema.

Aliongeza licha ya yeye kuwa mstaafu wa umoja wa mataifa bado wanamfuatilia katika shughuli za kimaendeleo ambazo anazifanya akiwa ndani na nje ya nchi.

"Kama ukijikwaa, ukianguka na kusimama watu wanaangalia kulikoni, na huu ni utamaduni wao, kwa hiyo pale uongo na fitina havina nafasi," alisema kwa msisitizo wakati akizungumza na wanahabari.


Diwani wa Kata ya Karambi ambaye pia ni Mjumbe wa mkutano Mkuu wa Taifa wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM),  Felix Bwahama ambaye aliongozana na  Profesa Tibaijuka alishukuru UN kwa kumtunuku tuzo hiyo ambapo alisema ni fahari kwa wanakagera na taifa kwa ujumla licha ya baadhi ya watu nchini kubeza kazi anazizifanya ambazo zinaonekana kimataifa.
 Profesa Anna Tibaijuka akionesha cheti alichokabidhiwa sanjari na tuzo hiyo.
 Profesa Tibaijuka akisisitiza jambo katika mkutano huo na wanahabari. Kulia ni Mratibu wa mkutano huo, Mussa Ally.
 wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.


No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages