Gavana
wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Beno Ndulu (kushoto),
akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jioni
hii kuhusu kuchukuliwa kwa benki hiyo ambayo ilikuwa ikimilikiwa na
serikali kwa asilimia 100.
Mkurugenzi
wa Usimamizi wa Mabenki, Kenedy Nyoni (kushoto), akichangia jambo
kwenye mkutano huo. Kulia ni Gavana wa Benki Kuu, Profesa Beno Ndulu.
Meneja
Msaidizi Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki wa BoT, Victoria Msina
(kulia), akimkaribisha Gavana Beno Ndulu kuzungumza na wanahabari. Wa
pili kutoka kulia ni Kaimu Katibu wa Benki, Mustafa Ismail.
Waandishi wa habari wakichukua taarifa hiyo.
Wapiga picha wakiwa kazini.
Taswira ya ukumbi huo wakati wa mkutano.
Na Dotto Mwaibale
BENKI Kuu ya Tanzania (BoT), imechukua usimamizi wa Benki ya Twiga 9Twiga Bancop Limited) kuanzia Oktoba 2016 imefahamika.
Hayo
yamebainishwa na Gavana wa Tanzania, Profesa Beno Ndulu Dar es Salaam
leo jioni wakati akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari
kuhusu hatua hiyo ya kuchukuliwa kwa benki hiyo ambayo serikali ilikuwa
ikiimiliki kwa asilimia 100.
"Kwa
mamlaka iliyopewa benki kuu chini ya kifungu cha Sheria namba 56 (1)
(g) (i) na 56 (2) (a)-(d) cha Sheria ya mabenki na Taasisi za Fedha ya
mwaka 2006 benki kuu ya Tanzania imeamua kuchukua usimamizi wa benki
hiyo kuanzia tarehe 28 Oktoba 2016" alisema Ndulu.
Alisema
uamuzi huo umechukuliwa baada ya kubaini kuwa benki hiyo ina upungufu
mkubwa wa mtaji kinyume na matakwa ya sheria ya Mabenki na Taasisi za
Fedha ya mwaka 20016 na kanuni zake.
Alisema
upungufu huo wa mtaji unahatarisha usalama wa sekta ya fedha na pia
kuendelea kutoa huduma za kibenki kwa benki hiyo kutahatarisha usalama
wa amana za wateja wake.
Profesa
Ndulu alisema kutokana na uamuzio huo Benki Kuu ya Tanzania
imeisimamisha Bodi ya Wakurugenzi na Uongozi wa benki hiyo na imemteua
Meneja Msimamizi ambaye atakuwa na jukumu la kusimamia shughuli za benki
ya Twiga kwa kipindi ambacho itakuwa chini ya usimamizi wa benki kuu.
Alisema
pia Umma unaarifiwa kuwa katika kipindi kinachokadiriwa kufikia wiki
moja kuanzia siku ya taarifa hii, shughuli za utoaji wa huduma za
kibenki za benki hiyo zitasimama ili kutoa nafasi kwa ajili ya kupanga
taratibu za uendeshaji wa benki hiyo.
Alisema
Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuuhakikishia umma kuwa itaendelea
kulinda maslahi ya wenye amana katika mabenki kwa lengo la kuleta
ustahimilivu katika sekta ya fedha.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269