Breaking News

Your Ad Spot

Oct 1, 2016

KATIBU MKUU WA CCM, KINANA AKUTANA NA KATIBU MKUU WA CHAMA CHA CNDD-FDD CHA BURUNDI, JIJINI DAR ES SALAAM, LEO

Kataibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimkaribisha Katibu Mkuu wa Chama cha CNDD-FDD, Evariste Ndayishimiye, leo Oktoba 1, 2016, katika Ofis Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kuwa na mazungumzo baina ya viongozi hao kuhusu uhusiano wa vyama hivyo ya CCM na CNDD-FDD. Kushoto ni Mnadhimu Mkuu wa CNDD-FDD, Gelase Ndabirabe.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mnadhimu Mkuu wa Chama cha CNDD-FDD,  Gerase Ndabirabe. Kushoto ni Kaimu Balozi wa Burundi nchini, Prefere Ndayishimiye
 Katibu  Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimsalimia Kaimu Balozi wa Burundi hapa nchini Prefere Ndayishimiye  alipokuwa akiupokea ugeni huo wa Katibu Mkuu wa CNDD-FDD
 Msemaji wa CCM Christopher Ole Sendeka akisalimiana na Katibu Mkuu wa chama cha CNDD-FDD cha Burundi Evariste Ndayishimiye ugeni wa Katibu mkuu huyo ulipowasili leo Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Dar es Salaam. Wapili kulia ni Balozi David Kapya. 
 Kataibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpeleka Ofisini kwake, Katibu Mkuu wa Chama cha CNDD-FD cha Burundi baada ya kuwasili kwa ajili ya mazungumzo. Kushoto ni Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka 
 Kataibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpeleka Ofisini kwake, Katibu Mkuu wa Chama cha CNDD-FD cha Burundi baada ya kuwasili kwa ajili ya mazungumzo.
 Kataibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkaribisha kuketi kwa ajili ya kuendelea na mazungumzo, Ofisini kwake, Katibu Mkuu wa Chama cha CNDD-FD cha Burundi baada ya kuwasili kwa ajili ya mazungumzo hayo leo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Kulia ni Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka
 Kataibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu Mkuu wa Chama cha CNDD-FD cha Burundi wakifurahia jambo wakati wa mazungumzo yao katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo 
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na ujumbe wake, akiwa katika mazungumzo na Katibu Mkuu wa chama cha CNDD-FDD Evariste Ndayishimiye na ujumbe wake, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya maofisa katika ujumbe wa Burundi uliofuatana na Katibu Mkuu wa Chama cha  CNDD-FDD Evariste Ndayishimiye, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam. PICHA ZAIDI/BOFYA HAPA

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages