.

RAIS DK. MAGUFULI AAGANA NA KIONGOZI MKUU WA MADHEHEBU YA BOHORA DUNIANI, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM, LEO

Oct 13, 2016

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin Ikulu jijini Dar es salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea mfano wa moja ya Hundi ya USD 100,000, kutoka kwa kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin aliyechangia jumla ya kiasi cha dola za Kimarekani 250,000/- kwa ajili ya waathirika wa Maafa ya Tetemeko lililotokea mkoani Kagera. Kulia ni Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa.
 Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin akiwaombea dua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Ikulu jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika picha ya pamoja na Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª