Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati
ya Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Ukraine hapa nchini Yevhemsi
Tsymbalik Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati
ya Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Ghana hapa nchini Kwame
Asamoah Tenkorang Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru
Balozi mteule wa Ghana hapa nchini Kwame Asamoah Tenkorang mara baada ya
kupokea Hati yake za Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana
jambo na Balozi mteule wa Ghana hapa nchini Kwame Asamoah Tenkorang
Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati
ya Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Jamhuri ya Sudan Mahjoub
Ahmed Abdallah Sharfi Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika
picha ya pamoja na Balozi mteule wa Jamhuri ya Sudan hapa nchini Mahjoub
Ahmed Abdallah Sharfi mara baada ya kupokea Hati yake ya utambilisho
Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na
Balozi mteule wa Jamhuri ya Sudan hapa nchini Mahjoub Ahmed Abdallah
Sharfi mara baada ya kupokea Hati yake ya utambilisho Ikulu jijini Dar
es Salaam
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana
jambo na Balozi mteule wa Jamhuri ya Sudan hapa nchini Mahjoub Ahmed
Abdallah Sharfi mara baada ya kupokea Hati yake ya Utambulisho Ikulu
jijini Dar es Salaam.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiaagana na
Balozi mteule wa Jamhuri ya Sudan hapa nchini Mahjoub Ahmed Abdallah
Sharfi mara baada ya kupokea Hati yake ya Utambulisho Ikulu jijini Dar
es Salaam.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru
Balozi mteule wa Ukraine hapa nchini Yevhemsi Tsymbalik mara baada ya
kupokea Hati yake ya Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na
Balozi mteule wa Ukraine hapa nchini Yevhemsi Tsymbalik mara baada ya
kupokea Hati yake ya Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati
ya Utambulisho kutoka kwa balozi mteule wa Jamhuri ya Slovakia Frantisek
Dlhopolcek Ikulu jijini Dar es Salaam
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru
balozi mteule wa Jamhuri ya Slovakia hapa nchini Frantisek Dlhopolcek
mara baada ya kupokea Hati yake ya Utambulisho Ikulu jijini Dar es
Salaam.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana
jambo na balozi mteule wa Jamhuri ya Slovakia hapa nchini Frantisek
Dlhopolcek mara baada ya kupokea Hati yake ya Utambulisho Ikulu jijini
Dar es Salaam.
Picha na Ikulu.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amepokea hati za utambulisho za mabalozi wanne
wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini.
Mabalozi
waliowasilisha hati zao za utambulisho Ikulu Jijini Dar es Salaam ni
Balozi wa Jamhuri ya Sudan hapa nchini Mhe. Mahjoub Ahmed Abd Allah
Sharfi, Balozi wa Jamhuri ya Slovakia hapa nchini Mhe. Frantisek
Dlhopolcek, Balozi wa Ukraine hapa nchini Mhe. Yevheni Tsymbaliuk na
Balozi wa Jamhuri ya Ghana Mhe. Kwame Asamoah Tenkorang.
Rais
Magufuli amezungumza na Mabalozi hao kwa nyakati tofauti baada ya
kupokea hati zao za utambulisho, ambapo wamesisitiza umuhimu wa
kuendeleza na kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na
nchi hizo kwa kujikita zaidi katika biashara na uwekezaji.
"Mhe.
Balozi najua nchi yenu ya Sudan ina utajiri wa mafuta na imefanikiwa
kujenga uchumi wake kupitia mafuta, sisi pia hapa nchini tumebaini uwepo
wa mafuta na gesi asilia katika maadhi ya maeneo, ningependa uhusiano
na ushirikiano wetu sasa ujielekeza katika kubadilishana uzoefu na ujuzi
wa namna tunavyoweza kunufaika na mafuta na gesi" amesema Rais Magufuli
alipokuwa akizungumza na Balozi wa Sudani hapa nchini Mhe. Mahjoub
Ahmed Abd Allah Sharfi.
Dkt.
Magufuli pia ametoa wito kwa wafanyabiashara na wawekezaji kutoka nchi
za Sudan, Slovakia, Ukraine na Ghana kuja kuwekeza hapa nchini katika
sekta mbalimbali zikiwemo Mafuta na gesi, Kilimo, Uvuvi, Mbuga za
wanyama, Madini na ufugaji.
"Hivi
sasa Tanzania ipo katika mpango wa ujenzi wa viwanda na pia tunatekeleza
mpango wa pili wa maendeleo, hivyo nakuomba Mhe. Balozi uwahamasishe
wafanyabiashara na wawekezaji wa Ukraine waje wawekeze katika viwanda
kwani soko la uhakika la bidhaa lipo" amesisitiza Dkt. Magufuli
alipokuwa akizungumza na Balozi wa Ukraine hapa nchini Mhe. Yevheni
Tsymbaliuk.
Aidha,
Rais Magufuli amewasihi Mabalozi wa Slovakia, Ukraine na Ghana ambao
makazi yao ya Ubalozi yapo Mjini Nairobi nchini Kenya kuanzisha Ubalozi
wao hapa nchini ili kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano katika
masuala ya biashara na uwekezaji.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
10 Oktoba, 2016.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269