Breaking News

Your Ad Spot

Oct 12, 2016

TAASISI YA TIBA YA MIFUPA MUHIMBILI MOI YAFANYA UPASUAJI MKUBWAKWA MAFANIKIO


 Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI), Dar es Salaam, kwa mara ya kwanza imefanya upasuaji mkubwa kwa mafanikio makubwa wa kunyoosha mfupa wa mgongo wa mtoto uliopinda (Kibiongo) kitaalamu (Scoliosis).

Upasuaji huo umefanyika kwa kutumia technolojia ijulikanayo kama ‘Posterior Instrumentation and Fusion’ ambayo inahusisha uwekaji wa vyuma maalum kwenye mfupa wa mgongo uliopinda katika sehemu ya juu na chini ya mfupa wa mgongo  na kuufanya mgongo unyooke inavyotakiwa.

Taassisi ya MOI imefanikiwa kufanya upasuaji huo  kupitia madaktari bingwa wa MOI walioko kwenye mafunzo ya ubobezi wa juu katika upasuaji wa mifupa na mgongo kwa watoto  kwa kushirikiana na madaktari bingwa kutoka Marekani.

Aidha, Uanzishwaji wa upasuaji huu umetokana na kuanzishwa kwa ushirikiano wa kimafunzo kati ya Taasisi ya MOI na Chuo cha madaktari bingwa wa upasuaji cha Afrika Mashariki , Kati na Kusini ‘COSECSA’ na Madaktari bingwa kutoka Marekani.

Uanzishwaji wa upasuaji huu wa kunyoosha migongo ya watoto iliyopinda (Scoliosis) unatarajiwa kuisaidia serikali kupunguza rufaa za kuwapeleka wagonjwa nje ya nchi ambazo ni za gharama kubwa. Ambapo gharama za kumtibu mtoto mmoja nje ya nchi ni zaidi ya dola za kimarekani elfu 30 hadi 40.

Hivyo, Uongozi wa Taasisi ya MOI unatoa wito kwa madaktari kwote nchini kuja kupata mafunzo hayo hapa MOI, Pia wazazi wenye watoto wenye matatizo hayo wawalete hospitali ili wafanyiwe uchunguzi na upasuaji

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages