Breaking News

Your Ad Spot

Oct 3, 2016

WATU KADHAA WAFARIKI DUNIA KATIKA MAKABILIANO ETHIOPIA

media
Waandamanaji wakidai mwisho wa ukandamizaji dhidi ya watu kutoka jamii ya Oromo, mjini Addis Ababa, Agosti 6, 2016.
Makabiliano kati ya polisi na waandamanaji yamesababisha watu wengi kufariki dunia nchini Ethiopia, wakati wa tamasha la jadi la Oromo Ireecha. Tukio hilo limetokea Jumapili asubuhi katika mji wa Bishoftu, kusini mwa mji wa Addis Ababa, lakini taarifa ya watu waliopoteza maisha bado haijathibitishwa na serikali.
Ni vigumu kusema kwa sasa ni watu wangapi wamepoteza maisha Jumapili hii asubuhi katika mji wa Bishoftu mkoani Oromo, jina la kabila la kwanza kwa watu wengi nchini Ethiopia. Makabiliano yalilipuka wakati wa sikukuu ya kidini inayoashiria mwisho wa msimu wa mvua.
Umati wa watu waliokuepo katika sherehe hizo walipinga uwepo wa viongozi kutoka jamii ya Oromo wanaoshirikiana na serikali, ambao wanawachukulia kama wasaliti. Waandamanaji walijaribu kuvamia jukwaa waliokuemo viongozi hao, lakini polisi walijibu kwa mabomu ya machozi.
Ilifuatiwa hali ya wasiwasi na hofu na kusababisha watu kukanyagana ambapo wakati huo watu kadhaa walipoteza maisha. Mpiga picha wa shirika la habari la AFP anasema aliona miili angalau ishirini ya watu waliofariki.
Upinzani nchini Ethiopia kwa upande wake, unadai kuwa watu zaidi ya 100 walifariki katika mkanyagano huo. Tamasha lilivunjwa na tukio hili linakumbusha hali ya mivutano inayoshuhudiwa katika mkoa wa Oromo wakati ambapo maandamano dhidi ya serikali ambayo yalianza karibu mwaka mmoja uliyopita yameendelea kushika kasi.
Kwenye mitandao ya kijamii, wanaharakati kutoka jamii ya Oromo wametoa wito wa hasira wa siku tano, huku idadi kubwa ya polisi ikionekana Jumapili hii mchana katika mkoa wa Oromo na karibu ya mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa.RFI

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages