Breaking News

Your Ad Spot

Oct 6, 2016

WAZIRI MKUU KUKUTANA NA WAFANYABIASHARA SOKO LA SABASABA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameahidi kukutana na wafanyabiashara wa soko la Sabasaba mkoani Dodoma ili kuzungumzia namna ya kulikarabati na kulifanya liwe la kisasa.Amesema miongoni mwa mambo watakayoyajadili katika kikao hicho ambacho hakutaja siku ni pamoja na kuboresha mazingira ya kufanyia biashara hasa kwa wanaouza bidhaa nje ya maduka.Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumatano, Oktoba 5, 2016) wakati alipotembelea maduka hayo yaliyoko katika barabara ya One Way inayopita katikati ya barabara ya sita hadi ya 11 pamoja na soko la Sabasaba akiwa kwenye ziara ya kukagua maeneo ya kutolea huduma za jamii mjini Dodoma.
Amesema Serikali tayari imeshahamia Dodoma hivyo wafanyabiashara wanatakiwa kutumia fursa hiyo kwa kuboresha biashara zao ili waweze kumudu ushindani wa soko.
“Wafanyabiashara lazima mboreshe biashara zenu, muongeze usafi zaidi na ikiwezekana muimarishe majengo yenu yawe ya kisasa zaidi kwani haiwezekani maduka ya Makao Makuu ya Nchi yawe katika hali hii,” amesema.
Pia Waziri Mkuu amewataka wafanyabiashara hao wasiogope kwenda kukopa katika taasisi mbalimbali za kifedha kwa lengo la kujiongeza mitaji na kupanua biashara.Amesema tayari alishatoa maagizo kwa wamiliki wa benki kuhakikisha wanawawezesha wajasiriamali wadogo kwa kuwapa mikopo, hivyo aliwataka wasiogope na badala yake wachangamkie fursa hiyo.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
S. L. P. 980,
DODOMA.
JUMATANO, OKTOBA 05, 2016

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages