Breaking News

Your Ad Spot

Oct 1, 2016

WAZIRI NAPE AFUNGUA MAONYESHO YA UTAMADUNI WA CHINA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Nape akizungumza leo
Na Genofeva Matemu, WHUSM
Ushirikiano wa Kidiplomasia kati ya Tanzania na China katika nyanja mbalimbali zikiwemo za Sanaa na Utamaduni umekuwa chachu kubwa katika kuwajengea uwezo wasanii na kutekeleza shughuli za kimaendeleo zinazofanywa na wataalamu kutoka pande hizi mbili.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokua akizindua wiki ya Maonyesho ya Utamaduni wa China katika Ukumbi wa Utamaduni wa watu wa China leo jijini Dar es Salaam.

 “Kwa miaka mingi Tanzania na China zimekuwa na ushirikiano uliotoa fursa kwa watu wake kujifunza shughuli za sanaa na kiutamaduni zilizoko katika kila nchi hivyo kuendeleza na kuuenzi ushirikiano uliopo katika sekta za Sanaa na Stamaduni” amesema Mhe. Nnauye

Mhe. Nnauye amesema kuwa ushirikiano wa nchi hizi mbili umeweza kukua, kuboresha na kuendeleza wasanii wetu hasa katika kipindi hiki cha maonyesho ambapo hutoa nafasi kwa wasanii wa Tanzania kujifunza mambo mbalimbali ya kiutamaduni na kuwapa wasanii wa hapa nchini fursa ya kufanya maonyesho kama haya nchini China.

Kwa upande wake Kaimu Balozi wa China nchini Tanzania Bw. GOU Haodong amesema kuwa Maonyesho ya Utamaduni wa China hapa nchini yanatoa fursa nzuri kwa wananchi wa Tanzania kuelewa na kujifunza utamaduni na sanaa ya China, kuimarisha ushirikiano wa utamaduni wa China na Tanzania pamoja na kukuza urafiki wan chi hizi mbili.

Naye Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Utamaduni kutoka Jiangxi China Bw. Chen Hongmin amesema kuwa China itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kubadilishana uzoefu kwa sekta ya Sanaa na Utamaduni na kujifunza mambo mapya ili kuendeleza Utamaduni, ushirikiano na uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizi mbili.

Wiki ya Maonyesho ya Utamaduni wa China itakuwa na maonyesho mbalimbali kama vile maonyesho ya sarakasi ya Kichina, maonyesho ya picha, hadhara za opera za China, Udaktari wa kijadi wa China na Utamaduni wa mazoezi maalumu yanayojenga afya yaitwayo Qigong.PICHA ZA TUKIO HILI/>>BOFYA HAPA

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages